9 Oktoba 2025 - 21:49
Si jambo lisilowezekana Israel kuishambulia Saudia; Riyadh imo ndani ya mradi wa ‘Israel Kubwa

Kutoa matrilioni ya dola kwa Trump na kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel hakukuwaletea usalama wowote Saudia na washirika wake.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Houthi ametanabahisha kwamba Si jambo lisilowezekana Israel kuishambulia Saudia; Riyadh imo ndani ya mradi wa ‘Israel Kubwa”.

Muhammad Ali al-Houthi, mjumbe wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen, katika mahojiano na kituo cha televisheni cha al-Masirah, alisema:

Hatuoni kama jambo lisilowezekana Israel kuishambulia Saudia, kwani Saudia imo ndani ya mradi wa Israel Kubwa.

Marekani inamchukulia utawala wa Kizayuni (Israel) pekee kuwa mshirika wake wa kweli, na nchi ambazo zimelipa mabilioni ya dola zinachukuliwa na Washington kuwa zimefanya tu wajibu wao. Kutoa matrilioni ya dola kwa Trump na kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel hakukuwaletea usalama wowote Saudia na washirika wake.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha