Kwa mujibu wa Shirika la habari la Ahl al-Bayt (AS) - Abna - Kamati ya Ijtihad na Fat'wa katika Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Duniani imeeleza huzuni na masikitiko yake kutokana na kuendelea jinai na mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza chini ya uungaji mkono wa Marekani na katika kivuli cha ukimya wa Jumuiya za Kimataifa na nchi za Kiislamu na Kiarabu.
1. Wajibu wa Jihad: Kusisitiza juu ya Fatwa iliyotangulia, Jihad dhidi ya utawala wa Kizayuni na mamluki na askari wake ambao wanahusika katika mauaji ya halaiki ya watu wa Gaza katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu ni wajibu madhubuti (na Mutlaki). Kwanza, itakuwa ni wajibu kwa watu wa Palestina, kisha kwa nchi jirani kama vile Misri, Jordan na Lebanon, na kisha kwa nchi zote za Kiislamu.
2. Ni haramu kumsaidia adui: Ni haramu kumsaidia adui kafiri kuwaua Waislamu wa Ghaza kwa njia yoyote ile. Kuanzia uuzaji wa silaha hadi ruhusa ya kupita kwenye Mfereji wa Suez, Bab al-Mandab, Mlango-Bahari wa Hormuz au njia nyingine yoyote ya bahari, nchi kavu au angani.
3. Utakatifu wa kutoa mafuta, chakula na mahitaji: Ni marufuku kutoa mafuta, gesi, chakula na bidhaa zozote zinazotumika katika vita dhidi ya Gaza. Yeyote anayefanya hivi kwa kuupenda utawala wa Kizayuni au uadui na upinzani wa Kiislamu anahesabiwa kuwa ni murtadi.
4. Umuhimu wa kuunda muungano wa kijeshi wa Kiislamu: Nchi za Kiislamu lazima ziunde muungano wa kijeshi wa haraka na wa umoja ili kulinda ardhi na watu wao wa Kiislamu.
5. Marekebisho ya mikataba na utawala wa Kizayuni: Nchi za Kiislamu ambazo zina mapatano na utawala unaoukalia kwa mabavu Palestina zinapaswa kuyapitia upya mapatano hayo, na kuchukua msimamo madhubuti iwapo mapatano hayo yatakiuka na utawala huo wa kizayuni.
6. Wajibu wa Jihad ya Kifedha (Mali): Ni wajibu kwa matajiri watoe kutoka katika mali zao (si Zakat tu) kwa ajili ya kuwaandalia Mujahidina na kusaidia familia za Mashahidi.
7. Kuidhinisha na kuhalalisha uhusiano na utawala wa Kizayuni: Uhusiano wowote na utawala unaoukalia Palestina kwa mabavu ni haramu na nchi za Kiislamu ambazo zimenaufanya uhusiano huo zinalazimika kukata uhusiano wao na Israel.
8. Wajibu wa Wanachuoni: Wanachuoni wana wajibu wa kuvunja ukimya, kutangaza ulazima wa Jihadi dhidi ya utawala unaoikalia Palestina kwa mabavu, na kuwawekea shinikizo watawala na majeshi kutimiza wajibu wao wa kidini na kihistoria.
9. Umuhimu wa kuwekewa vikwazo kamili: Vikwazo vya kisiasa (kukata uhusiano wa kidiplomasia), kiuchumi (vikwazo vya kununua vifaa kutoka kwa adui), vikwazo vya kitamaduni na kisayansi ni muhimu, na uwekezaji katika makampuni yanayojenga makazi ya Wazayuni lazima usitishwe.
10. Wito kwa Serikali ya Marekani: Kuhutubia / kutoa wito kwa utawala wa Trump, ambao uliahidi kuunga mkono Gaza, na kutoa wito kwa Waislamu wa Marekani kutoa shinikizo la kisiasa kwa Serikali yao.
11. Kuendelea kuyawekea vikwazo makampuni yanayounga mkono utawala wa Kizayuni: Kazi hii imekuwa na ufanisi na inapaswa kuendelezwa hasa dhidi ya nchi zinazoupa silaha utawala huo moja kwa moja.
12. Usaidizi wa watu wa Gaza: Waislamu wanapaswa kutoa mahitaji ya chakula, dawa na mafuta kwa watu wa Gaza kwa njia yoyote inayowezekana. Serikali zikizuia, basi kumtii Mwenyezi Mungu katika kuunga mkono walioonewa na kudhulumiwa kunatanguliza kuliko kuwatii watu (na serikali zao).
13. Umoja wa Waislamu: Umoja wa Waislamu kwa sasa unahitajika zaidi kuliko wakati mwingine wowote, kuweka kando tofauti, umoja wa makundi ya Wapalestina, Serikali na Taasisi za Kiislamu ni wajibu.
14. Dua kwa ajili ya Gaza: Watu wanapaswa kuwaombea ushindi watu wa Gaza katika sala na dua, hasa katika Nawafil (Sala za Sunna) na Wajibati (Sala za Wajibu), na waombe msaada kwa Mwenyezi Mungu katika hali zote.
15. Kuwashukuru wafuasi na watetezi wa watu wa Gaza: Mwishoni, shukrani zimetolewa kwa nchi, taasisi, watu binafsi na hata Wayahudi ambao wameunga na wanawaunga mkono watu wa Gaza.
Your Comment