Ni wajibu kwa Waislamu kote duniani kuwafanya maadui hawa wajute kwa matamshi na vitendo vyao. Na ikiwa Waislamu watapata mashaka au hasara kutokana na kusimama dhidi yao, basi wao watakuwa na thawabu ya mujahid (mpiganaji katika njia ya Mwenyezi Mungu), Insha'Allah.
Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Ulimwenguni umetoa Fat'wa kuhusu Wajibu wa Jihadi katika kuunga mkono Ghaza na kusisitiza kuwa, Jihadi dhidi ya utawala wa Kizayuni na mamluki na askari wake wanaohusika na mauaji ya halaiki ya watu wa Ghaza katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina ni wajibu mutlaki (unaomgusa kila mtu).