23 Aprili 2025 - 22:08
Dr. Ali Taqavi, Mwakilishi wa Jamiat Al-Mustafa (s)Tanzania, akiambatana na Sheikh Dr. Alhad Mussa Salum watembelea uwanja wa Michezo Zanzibar + Picha

Uislamu umesisitiza Umoja wa Kiislamu, na madhehebu yote ya Kiislamu yanaunganishwa na Umoja wa Kiislamu, na Kibla cha Waislamu wote ni kimoja, na Qur'an ndio Kitabu chao na Muongozo wao.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Dr. Ali Taqavi, Mwakilishi wa Jamiat Al-Mustafa (s) - Dare-salam, Tanzania, akiambatana na Sheikh Dr. Alhad Mussa Salum, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), walifanya ziara muhimu Zanzibar, Tanzania. Katika Ziara hii muhimu, walipata fursa ya kumtembelea Mheshimiwa Mufti wa Zanzibar, Mufti Mkuu Wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, na Sheikh Abdu, Kiongozi Mwakilishi wa Bakwata nchini Zanzibar. Katika katika Kikao na Mheshimiwa Mufti wa Zanzibar, walijadiliana kuhusiana na maadalizi ya Utangulizi wa Tamasha la Qur'an. Kikao hiki hiki kilijiri na kuwa na mashauriano yenye mafanikio makubwa. Mheshimiwa Mufti wa Zanzibar, alifurahi na kuonyesha kufurahishwa na ziara hiyo na mazungumzo yaliyijiri baina yao aliyasifu kuwa ni mazungumzo muhimu kwa ajili ya maendeleo ya Uislamu na Uislamu. 

Dr. Ali Taqavi, Mwakilishi wa Jamiat Al-Mustafa (s)Tanzania, akiambatana na Sheikh Dr. Alhad Mussa Salum watembelea uwanja wa Michezo Zanzibar + Picha

Azimio na Hitimisho la Mazungumzo hayo yenye faida ni hili kuwa Tamasha hilo la Qur'an Tukufu lifanyike katika uwanja wa Michezo - Zanzibar, Tanzania (Insha Allah). Na Mgeni rasmi wa Tamasha hilo la Qur'an Tukufu anatarajiwa kuwa ni Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Dr.Hussein Mwinyi. Samahat Sheikh Dr. Alhad Musa Salum aliambata na Hojjat Al-Islam wal - Muslimin , Dr. Ali Taqavi kwenda kuuona na kuukagua uwanja wa mkubwa wa Michezo wa Zanzibar, panapotarajiwa kufanyika kwa Tamasha kubwa la Qur'an Tukufu.

Dr. Ali Taqavi, Mwakilishi wa Jamiat Al-Mustafa (s)Tanzania, akiambatana na Sheikh Dr. Alhad Mussa Salum watembelea uwanja wa Michezo Zanzibar + Picha

Aidha, Samahat Sheikh Abdu, Kiongozi Mwakilishi wa "BAKWATA" nchini Zanzibar, na Samahat Sheikh Dr. Alhad Mussa Salum, walipata fursa adhimu ya kutembelea Chuo cha Qur'an Tukufu cha Jamiat Al-Mustafa (s) kilichopo Zanzibar - Tanzania. wote kwa pamoja walipata fursa ya kuzungumza na wanafunzi wa chuo hiki na kuwapa nasaha muhimu na maridhawa za kielimu. Pia walisisitiza juu ya Umoja wa Kiislamu na kubainisha kuwa madhehebu yote ya Kiislamu yanaunganishwa na Umoja wa Kiislamu na Kibla cha Waislamu wote ni kimoja na Qur'an ndio Kitabu chao na Muongozo wao.

Dr. Ali Taqavi, Mwakilishi wa Jamiat Al-Mustafa (s)Tanzania, akiambatana na Sheikh Dr. Alhad Mussa Salum watembelea uwanja wa Michezo Zanzibar + Picha

Dr. Ali Taqavi, Mwakilishi wa Jamiat Al-Mustafa (s)Tanzania, akiambatana na Sheikh Dr. Alhad Mussa Salum watembelea uwanja wa Michezo Zanzibar + Picha

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha