Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Hojjatul Islam Syed Hassan Zafar Naqvi, Naibu Kiongozi wa Majlis-e-Wahdat-e-Muslimeen Pakistan, amesema: "Ushindi na kushindwa ni wazi kabisa; wale waliofanya uchokozi sasa wamejificha kwenye makazi na mashimo, wakati wale ambao wameamua kufanya maamuzi ya kujibu mashambulizi wapo barabarani wakitoa nara za "Allah Akbar - Mwenyezi Mungu Mkubwa".
Ameongeza kuwa: "Msimamo wa Serikali ya Pakistan katika kuunga mkono nchi ndugu ya Kiislamu ya Iran ni hatua ya kijasiri na ya kupongezwa. Sawa na Iran na Pakistan zinavyosimama bega kwa bega, nchi nyingine za Kiislamu ikiwemo Saudi Arabia nazo zinapaswa kulaani waziwazi uchokozi wa Israel."
Naqvi alisisitiza: Iran na Pakistan ni tishio kubwa kwa Israel. Iran haitaki vita na uongozi wake umeepuka migogoro kadri inavyowezekana. Lakini wakati Israeli waoga inapoweka vita bila kuzingatia sheria za kimataifa, mwisho wa vita hivi pia utakuwa na Iran. Marekani na Israel zinaogopa kifo, huku Wairan wakichukulia kifo kwa ajili ya haki kuwa ni heshima kubwa.
Akizungumzia nafasi ya mambo ya ndani amesema: "Lau makundi ya wanafiki ndani ya Iran yasingewasaidia adui, mashambulio ya Israel yangefeli kabisa. Mara tu mashambulizi ya Iran yatakapozidi, kilio cha Israel kitasikika na kila mtu."
Naqvi alionya: Marekani na waitifaki wake hivi karibuni watatafuta hifadhi katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili kuihami Israel, na walimwengu wataona jinsi baraza hilo linavyojaribu kuuunga mkono utawala huo wa Kizayuni kwa njia ya kejeli.
Your Comment