Sheria
-
Baraza Kuu la Fat'wa la Syria: Kusaliti na kuomba msaada kwa adui wa Kizayuni ni haramu
"Adui wa Kizayuni ni adui wa wazi na ambaye uadui wake umethibitika, na kuomba msaada kwake ni miongoni mwa mambo yaliyo haramu kwa yakini."
-
A'shura ni ishara ya uvumilivu katika vyombo vya habari vya Bahrain, lakini kwa kweli, ni eneo la ukandamizaji dhidi ya Mashia
Mwanaharakati wa haki za binadamu wa Bahrain amesema: A'"shura inatolewa kila mwaka katika vyombo vya habari vya Bahrain kama ishara ya uhuru na uvumilivu wa kidini, lakini kivitendo wafuasi wa Kishia wanakabiliwa na ukiukwaji mkubwa wa sheria na vikwazo vikali, kuanzia kukamatwa na kuandikiwa wito hadi kuharibiwa maeneo ya kidini na mashinikizo ya kubadili mavazi ya kidini.
-
Nchi 11 zalaani uvamizi wa Israel dhidi ya Iran katika kikao cha Baraza la Magavana
Katika taarifa ya nchi kumi na moja wanachama wa Bodi ya Magavana, inachukulia kuwa "shambulio lolote la silaha au tishio dhidi ya vituo vya nyuklia vinavyotolewa kwa madhumuni ya amani ni ukiukaji wa kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa, sheria za kimataifa na Mkataba wa Shirika la IAEA."
-
Mwanazuoni wa Kishia wa Pakistani:
Uungaji mkono wa Serikali ya Pakistan kwa Iran ni hatua ya kijasiri na ya kupongezwa
Katibu Mkuu wa Baraza la Umoja wa Waislamu wa Pakistan amepongeza uungaji mkono wa serikali ya Pakistan kwa Iran dhidi ya mashambulizi ya Israel na ameitaja hatua hiyo kuwa ya kijasiri na ya kupongezwa na kuzitaka nchi za Kiislamu kuchukua misimamo thabiti dhidi ya uvamizi wa Wazayuni.
-
Ahkam za Kisheria kwa Mujibu Ahlul-Bayt (a.s):
Hukumu za Kisheria zitakazomfanya Mwanadamu afaulu Kesho Siku ya Kiyama
Hukumu za Kiislamu zinakutaka Muislamu Itikadi yako iwe ni Itikadi sahihi. Na Uislamu unatufndisha kuwa haijuzu kwa Muislamu yeyote kumfuata (Kumqalid) mtu kuhusiana na suala la Kiitikadi, kwa maana kwamba: Lolote linalohusiana na itikadi, inabidi Muislamu ulikubali na kuliitikadia kwa kutegemea dalili na uthibitisho madhubuti ima wa: Qur’an Tukufu, au Hadithi na Sunna za Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake na Aali zake) na Riwaya mbalimbali za Maimam watoharifu (amani iwe juu yao), au uwe ni uthibitisho unaotokana na dalili za kiakili.