Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul Bayt (as) -ABNA-, nchi kumi na moja wanachama wa Bodi ya Magavana zilitoa taarifa ya pamoja kulaani mashambulizi ya kijeshi ya utawala wa Israel dhidi ya vituo vya amani vya nyuklia vya Iran kuwa ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa na kutaka Wakala na Baraza la Usalama kuchukua hatua za haraka kukabiliana na kurudiwa kwa uchokozi huo.
Taarifa hiyo iliyosomwa katika kikao kisicho cha kawaida cha Baraza la Magavana inasema: "Tunalaani hujuma za utawala wa Israel dhidi ya Iran, ikiwemo mashambulizi ya kijeshi dhidi ya vituo vya nyuklia chini ya ulinzi wa IAEA, ambayo ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa, Mkataba wa Umoja wa Mataifa na Mkataba wa IAEA."
Taarifa hiyo iliongeza: "Tunaamini kwa dhati kwamba mashambulizi haya ya kijeshi, pamoja na kutishia amani na usalama wa kimataifa, yanadhoofisha imani katika Mkataba wa Kuzuia Kueneza Silaha za Nyuklia (NPT), yanajumuisha kupuuza kwa wazi mfumo wa ulinzi wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki, na kuhatarisha maendeleo zaidi ya nishati ya nyuklia kwa malengo ya amani."
Taarifa hiyo ilizingatia "shambulio lolote la silaha au tishio dhidi ya vituo vya nyuklia vinavyotolewa kwa madhumuni ya amani kuwa ukiukaji wa kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa, sheria za kimataifa na Mkataba wa Shirika la IAEA."
Your Comment