Iran, China na Urusi zimekosoa rasimu ya azimio dhidi ya Iran katika Baraza la Magavana la IAEA, zikisema ni ya kisiasa na inalenga kuongeza shinikizo badala ya kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, huku zikisisitiza kuwa hatua hizo zinaweza kuhatarisha diplomasia na utulivu wa nyuklia.
Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani, Hamas pia imewateua magavana wapya watano wenye uzoefu wa kijeshi kusimamia maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza, huku baadhi ya wapiganaji wake wakiwa tayari wametumwa kutekeleza majukumu hayo.