27 Aprili 2025 - 17:20
Udhalilishaji wa hivi karibuni wa mambo matukufu ya Waislamu wa Kisunni una nyanja tata zaidi

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kudumisha Umoja wa Madhehebu ya Kiislamu akilaani udhalilishaji wa mambo matukufu ya Waislamu wa Kisunni alisema: Udhalilishaji wa hivi karibuni una nyanja tata zaidi, na inatarajiwa kutoka kwa viongozi wa masuala haya kuchukua hatua za kuzuia kurudiwa kwa maafa kama haya.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AhlulBayt (a.s) — Abna — Hujjatul Islam Hamid Shahriari, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kudumisha Umoja wa Madhehebu ya Kiislamu, alitoa ujumbe akilaani udhalilishaji wa mambo matukufu ya Waislamu wa Kisunni katika kipindi kimoja cha televisheni.

Matni ya ujumbe huo ni kama ifuatavyo:

Udhalilishaji uliofanywa hivi karibuni dhidi ya baadhi ya mambo matukufu ya Waislamu wa Kisunni kwa hakika ulisababisha maumivu makubwa na huzuni isiyo na kifani.

Maumivu haya na huzuni vinatokana na mambo mawili: kwanza, kwamba kosa hili limewasababishia maumivu ndugu zetu Waislamu wa Kisunni — hasa maulamaa na wasomi wao — na pili, kwamba licha ya mafundisho yetu ya Kiislamu, Qur'ani na ya kimadhehebu, bado tunashuhudia vitendo vya kijinga vya kuchochea mifarakano, ambavyo bila shaka vinategemea fitna zinazopangwa au kuungwa mkono na maadui wa Uislamu.

Uzingatiaji wa Adabu za Kiislamu na Umuhimu wa Umoja wa Kiislamu

Kuzingatia adabu za Kiislamu ni jambo muhimu sana katika mafundisho halisi ya dini, na hili linajitokeza wazi katika mifano ya viongozi wa Kiislamu, wakiwemo Imam Ali (a.s.). Hata katika hali ngumu ya vita vya Siffin, Imam Ali alionyesha umakini mkubwa kuhusu suala hili na aliwakataza wanajeshi wake kutukana maadui kwa kusema:

 «إِنِّی أَکْرَهُ لَکُمْ أَنْ تَکُونُوا سَبَّابِینَ» (نهج البلاغه، خطبه ۲۰۶).


.Hakika mimi nachukia kuwa ninyi muwe ni watu wa matusi." (Nahjul Balagha, Hotuba ya 206)"

Mtazamo huu wa heshima na umoja umeendelea kuwa kipengele muhimu kwa Maimamu watakatifu (amani iwe juu yao) na kwa Wanazuoni wa Kiislamu, na umetumika kama mwongozo wa kiadili. Kwa mfano, Mwanzilishi wa Mfumo Mtukufu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Imam Khomeini (qaddasa sirrah), pamoja na mrithi wake, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, Khamenei (Mwenyezi Mungu Amhifadhi), wamekuwa wakitoa maonyo makali dhidi ya kauli yoyote inayoweza kufahamika kama dhihaka au dhihirisho la dhihaka kwa Maswahaba wa Mtume (s.a.w.w) na wake wa Mtume (s.a.w.w).

Kulinda Umoja wa Kiislamu na kujitahidi kutekeleza matakwa yake ni jambo la kimsingi, lakini katika hali ya sasa ambapo sehemu kubwa ya umma wa Kiislamu inakutana na machungu ya ukatili wa kinyama, umoja huu una umuhimu wa kipekee. Kwa hiyo, tunahitaji kutoa umuhimu wa ziada katika kushirikiana na kusaidiana ili kudumisha mshikamano.

Jumuiya ya Kimataifa ya Kudumisha Umoja wa Madhehebu ya Kiislamu, kwa kusisitiza maoni ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, inatoa wito kwa wahusika katika sekta ya utamaduni na vyombo vya habari kuwa na uangalizi mkubwa katika kufuata kanuni za kuunda umma mmoja wa Kiislamu. Uungaji mkono kwa msimamo huu lazima uwe sehemu ya shughuli zote za kitamaduni na kidini.

Mjadala wa taqrib (kujenga mshikamano na ukaribu kati ya Madhehebu za Kiislamu) ni kipengele muhimu cha maarifa ya Kiislamu. Inapaswa kuwa kipaumbele katika shughuli zote zinazohusu uhusiano wa Kiislamu na ulinzi wa umoja wetu. Tunapaswa kuepuka hatua yoyote inayoweza kuwapa nafasi maadui wa Uislamu kuanzisha mifarakano na ghasia.

Katika kipindi chote cha uhai wake, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa na hisia za kipekee kuhusu hatima ya ndugu Waislamu wa Kisunni katika nchi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu (na utawala haram na ghasibu wa kizayuni), na imetoa msaada mkubwa kwa makundi ya Muqawamah (mapambano ya upinzani dhidi ya udhalimu wa madhalimu na ukandamizaji), bila kujali madhehebu yao. Uungaji mkono wa Iran kwa makundi haya umeendelea kuleta wasiwasi kwa maadui wa Uislamu, na kwa hiyo, ni jambo la kawaida kwao kutumia kila fursa kuzuia mshikamano huu.

Kwa hiyo, kosa hili la kusikitisha linahitaji uangalizi wa kipekee na hatua madhubuti kutoka kwa wahusika, hasa viongozi wa vyombo vya habari, ili kuhakikisha kuwa makosa kama haya hayajirudii tena.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha