Mwenyekiti wa Baraza la Wanazuoni wa Kiislamu wa Bahrain alisisitiza kuwa kuacha njia ya Muqawama (mapambano dhidi ya wavamizi na dhulma) hakuzai chochote isipokuwa fedheha, udhalilishaji na utumwa.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kudumisha Umoja wa Madhehebu ya Kiislamu akilaani udhalilishaji wa mambo matukufu ya Waislamu wa Kisunni alisema: Udhalilishaji wa hivi karibuni una nyanja tata zaidi, na inatarajiwa kutoka kwa viongozi wa masuala haya kuchukua hatua za kuzuia kurudiwa kwa maafa kama haya.