Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Sambamba na maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad Al-Mustafa (S.A.W.W), sherehe yenye haiba na ya kiroho iliandaliwa katika Husainiyya ya Jumuiya ya Khoja Nchini Burundi. Hafla hiyo ilihudhuriwa kwa wingi na ndugu wa Kiislamu wa Madhehebu ya Sunni na Shia, ikionesha mshikamano na Umoja miongoni mwa Waislamu.
Katika mkusanyiko huo uliojaa nuru na baraka, wasemaji walisisitiza umuhimu wa Umoja kati ya Waislamu na kutaja "Wiki ya Umoja wa Kiislamu" kuwa ni fursa adhimu ya kuimarisha uhusiano wa kindugu kati ya wafuasi wa Madhehebu mbalimbali za Kiislamu.
Washiriki wa Sherehe hiyo pia walimuenzi Mtume Mtukufu (S.A.W.W) kwa heshima kubwa, na walieleza haja ya mshikamano, maelewano, na Umoja wa Umma wa Kiislamu katika kukabiliana na changamoto zinazoukabili ulimwengu wa Kiislamu kwa ujumla.
Kuandaliwa kwa hafla kama hii ni ishara ya kuishi kwa amani na kuheshimiana kati ya makundi tofauti ya jamii ya Kiislamu, jambo ambalo linaweza kuwa mfano bora wa kuimarisha mshikamano na muungano wa kitaifa na kimataifa.
Your Comment