Kiroho
-
Sheikh Hemed Jalala | Khutba ya Ijumaa (Malezi ya Watoto) - Masjidul Ghadir, Kigogo Post, Dar-es-Salaam
Sheikh Hemed Jalala alisisitiza umuhimu wa malezi bora ya watoto kwa kufuata misingi thabiti ya Kiislamu. Alibainisha kuwa familia ni msingi wa jamii, na hivyo malezi ya mtoto yanapaswa kuakisi maadili na mafundisho ya dini.
-
Kisomo cha Dua ya Kumail katika Hawza ya Hazrat Zainab (sa) – Kigamboni, Dar-es-Salaam
Hawza ya Hazrat Zainab (sa) iliyoko Kigamboni, Dar-es-Salaam, ni chuo makhsusi kwa ajili ya kuwalea mabinti wa Kiislamu kielimu na kimaadili. Chuo hiki kipo chini ya usimamizi wa Jamiat Al-Mustafa (s) – Tanzania, na mbali na masomo ya kielimu yanayotolewa humo, wanafunzi pia hupatiwa malezi ya kiroho kwa kupitia mafundisho ya dua na ibada.
-
Utafiti wa Kielimu – Nguzo ya Elimu ya Kudumu - Jamiat Al-Mustafa (s), Dar-es-Salaam - Tanzania
Mubahatha na Utafiti wa Kielimu ni moyo wa Elimu ya Kiislamu. Kupitia mijadala ya kielimu, Wanafunzi hubadilishana maarifa, kufungua milango ya utafiti, na kuimarisha uelewa wa kina wa masomo yao. Ukweli ni kwamba: Elimu bila Mubahatha ni kama mwili bila roho. Hupotea taratibu, na haidumu katika fikra za Mwanafunzi.
-
"Kuna Wivu wa Husuda na Wivu Ghibta | Je, Tuwe na Wivu wa Aina ya Ghibta au Tusiwe nao?"
Husuda ni kutamani neema ya mtu mwingine itoweke, iwe neema hiyo itamfikia mwenye husuda au la. Kinyume cha husuda ni 'Ghibta', ambapo mtu hatamani neema ya mwingine ipotee, bali anatamani kuwa na neema kama hiyo bila kumtakia mwingine mabaya.