8 Oktoba 2025 - 10:27
Ayatullah Nuri Hamedani: Leo, jambo kubwa zaidi la ma’rufu ni umoja kuzunguka mhimili wa Uongozi wa Mapinduzi na kulinda Mfumo wa Kiislamu

Ayatullah Nuri Hamedani amesisitiza kuwa: Kwa uwazi tunatambua kwamba Amr bil Ma’ruf na Nahy anil Munkar ni kati ya wajibu muhimu zaidi wa Kiislamu — au ndio wajibu muhimu zaidi — na hilo peke yake linatosha kuonyesha hadhi ya juu ya wajibu huu, hivyo haipaswi kuuchukulia kuwa jambo dogo.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Ayatullah al-Udhma Nuri Hamedani, mmoja wa Marjaa wakubwa wa Taqlid wa Kishia, ametuma ujumbe kwa mkutano wa kitaifa wa wafanyakazi, walimu na wakurugenzi wa Ofisi za Amr bil Ma’ruf wa al-Nahy anil Munkar, ulioandaliwa kwa kauli mbiu ya:
“Ushirikiano wa taasisi katika kufufua faradhi ya Amr bil Ma’ruf na Nahy anil Munkar nchini kote.”

Ujumbe huo ni kama ifuatavyo:

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمنِ الرَّحیمِ

الْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِینَ وَالصَّلَاةُ وَالسَّلَامُ عَلَی سَیِّدِنا وَنَبِیِّنَا أَبِی ‌الْقَاسِمِ المصطفی مُحَمَّد وَعَلَی أهلِ بَیتِهِ الطَّیِّبِینَ الطَّاهِرِینَ سیَّما بَقیَّهَ اللَّهِ فِی الأرَضینَ.

Salamu na heshima kwa mkutano huo mtukufu:

Moja ya masuala muhimu ambayo yanapaswa kupewa kipaumbele zaidi katika zama hizi na kufahamishwa vyema kwa jamii ni wajibu uliosahaulika wa Amr bil Ma’ruf wa al-Nahy anil Munkar (Kuanzisha mens na kukataza maovu). Ni wajibu ambao leo hii, kutokana na propaganda za maadui, au wakati mwingine kutokana na kutokufahamishwa vyema na marafiki, pamoja na ukosefu wa maarifa ya kutosha katika utekelezaji, umefanywa kuonekana kuwa ni jambo gumu katika jamii.

Ni wajibu ambao Qur’ani Tukufu imeueleza kuwa ni sababu ya mafanikio na wokovu wa binadamu, na imeutambua kuwa ni msingi wa furaha ya mwanadamu, pale inaposema:

«وَلْتَکُنْ مِنْکُمْ أُمَّةٌ یَدْعُونَ إِلَی الْخَیْرِ وَیَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَیَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْکَرِ وَأُولَئِکَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ»

Kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu, jambo linaloifanya Umma kuwa bora ni Amr bil Ma’ruf na Nahy anil Munkar. Takribani aya kumi za Qur’ani zimezungumzia wazi wajibu huu, na aya nyingi nyingine zimeashiria umuhimu wake.

Ni lazima kutambua kuwa katika kila jamii, ili kuidhibiti dhidi ya uovu, upotovu na maangamizi, ni muhimu kuwe na uangalizi wa kijamii na katika baadhi ya nyanja, uangalizi maalum. Haya yote yamepangwa kwa upana, kwa mpangilio na kwa mantiki ndani ya Uislamu chini ya mpango wa “ulazima wa majukumu mawili makubwa – Amr bil Ma’ruf na Nahy anil Munkar.”

Mpango huu, iwapo utatekelezwa ipasavyo, ni silaha yenye nguvu ya kung’oa mizizi ya ufisadi na ni nguzo imara ya kuelekeza mtu na jamii kuelekea ukamilifu wa kiroho na kimwili.

Kwa msingi huo, aya na hadithi nyingi zimewahimiza Waislamu kutekeleza majukumu haya mawili muhimu na kuzilinda kwa uangalifu. Hadi kufikia pale ambapo Mtume (s.a.w.w) amesema:

مَنْ أَمَرَ بِالْمَعْرُوفِ وَنَهَی عَنِ الْمُنْکَرِ فَهُوَ خَلِیفَةُ اللَّهِ فِی الْأَرْضِ وَ خَلِیفَةُ رَسُولِهِ وَ کِتَابه

(Yeyote anayefanya Amr bil Ma’ruf wa Al-Nahy anil Munkar ni Khalifa wa Mwenyezi Mungu duniani, na Khalifa wa Mtume Wake, na Khalifa wa Kitabu Chake.)

Hadithi hii inaonyesha kwamba majukumu haya mawili ni mpango wa kimungu, wa Mitume na wa Vitabu vya mbinguni. Mtu anayeyatekeleza (ikiwa masharti yamekamilika), anakuwa chini ya mwavuli wa mpango huu na anachukua hatua katika njia ya Mwenyezi Mungu — na cheo gani kilicho juu zaidi ya hicho!

Dalili bora ya umuhimu wa majukumu haya mawili ni kwamba ulinzi wa dini na jamii katika nyanja zote unategemea utekelezaji wake. Kwa maneno mengine, binadamu katika mwanga wa utekelezaji wa majukumu haya huokolewa na maangamizi na kuelekea kwenye kilele cha ukamilifu wa kibinadamu.

Majukumu haya mawili ndiyo dhamana ya utekelezaji wa wajibu wote wa kijamii, kiutamaduni, kisiasa na kiibada. Katika historia ya Uislamu, matokeo bora yaliyopatikana kupitia utekelezaji wa majukumu haya mawili ni mengi mno.

Miongoni mwa wajibu muhimu, mkubwa na wa juu zaidi katika Uislamu ni Amr bil Ma’ruf na Nahy anil Munkar. Kuhusu ukubwa wa hadhi ya majukumu haya, hakuna maelezo yaliyo wazi na kamili zaidi ya yale yaliyopokelewa kutoka kwa Ahlul Bayt (a.s).

ما ینبئک مثل خبیرHakuna atakayekujulisha vyema kama yule aliye mjuzi.

Sasa zingatia hadithi hizi mbili:

1_ Imam Ali (a.s) amesema:


وَ مَا أَعْمَالُ‏ الْبِرِّ کُلُّهَا وَ الْجِهَادُ فِی سَبِیلِ اللَّهِ عِنْدَ الْأَمْرِ بِالْمَعْرُوفِ وَ النَّهْیِ عَنْ الْمُنْکَرِ إِلَّا کَنَفْثَةٍ فِی بَحْرٍ لُجِّی‏


(Kazi zote njema, hata jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, zikilinganishwa na Amr bil Ma’ruf na Nahy anil Munkar, ni kama mate mbele ya bahari kubwa.)

2_Imam Sadiq (a.s) amesema:


إِنَ‏ الْأَمْرَ بِالْمَعْرُوفِ‏ وَ النَّهْیَ‏ عَنِ‏ الْمُنْکَرِ سَبِیلُ‏ الْأَنْبِیَاءِ وَ مِنْهَاجُ الصُّلَحَاءِ فَرِیضَةٌ عَظِیمَةٌ بِهَا تُقَامُ الْفَرَائِضُ وَ تَأْمَنُ الْمَذَاهِبُ‏ وَ تَحِلُّ الْمَکَاسِبُ وَ تُرَدُّ الْمَظَالِمُ وَ تُعْمَرُ الْأَرْضُ وَ یُنْتَصَفُ مِنَ الْأَعْدَاءِ وَ یَسْتَقِیمُ الْأَمْر

(Amr bil Ma’ruf na Nahy anil Munkar ni njia ya Mitume na mwenendo wa wacha Mungu; ni faradhi kuu kwa sababu kwa njia yake faradhi nyingine zote huimarishwa, njia huwa salama, biashara huwa halali, haki za watu hulindwa, ardhi hujengwa, kisasi huchukuliwa kutoka kwa maadui na mambo yote huwa sawa.)

Na mwanzoni mwa hadithi hiyo, majukumu haya mawili yameitwa أسمی الفرائض و أشرفها - wajibu wa juu na wa heshima zaidi.

Kwa kuzingatia kwamba faradhi ambayo kazi zote njema, hata jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, zinapolinganishwa nayo ni kama tone la maji mbele ya bahari kuu - faradhi ambayo kwa mwanga wake wajibu wote huimarishwa, njia huwa salama, biashara huwa halali, haki zinatekelezwa, uadilifu wa kijamii na kiuchumi unapatikana, ardhi hujengwa, na kisasi huchukuliwa kutoka kwa maadui wa dini - wale ambao hawakosi kufanya uovu juu yetu, bali hutamani tuendelee katika mateso na taabu; (alama za uadui wao ziko wazi katika maneno yao, na yaliyofichika mioyoni mwao ni makubwa zaidi).

Kwa hivyo, utekelezaji wa faradhi hizi mbili husababisha ufanisi katika nyanja zote za maisha.

Mwisho:
Kwa uwazi tunatambua kwamba Amr bil Ma’ruf wa al-Nahy anil Munkar ni wajibu muhimu zaidi wa Kiislamu - au kati ya wajibu muhimu zaidi. Hilo pekee linatosha kuthibitisha hadhi yake ya juu, hivyo haipaswi kuuchukulia kuwa jambo dogo.

Leo, jukumu la kwanza ni kutambua vyema ma’ruf na munkar katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.
Katika ulimwengu wa leo, munkar mkubwa zaidi ni uistikbari na uzayuni pamoja na wafuasi wao. Ndani ya nchi, ni mapambano dhidi ya ufisadi wa kiuchumi, kijamii na kitamaduni. Ikiwa leo kiongozi hatimizi wajibu wake, ni lazima kupaza sauti.

Ikiwa leo mtu anashambulia maslahi ya taifa na umoja wa wananchi, lazima akabiliwe. Ikiwa wajibu wa kidini kama Hijabu unadhoofishwa, haipaswi kukaa kimya.

Ikiwa leo maisha ya wananchi yanashikiliwa kama mateka wa malengo ya vyama na makundi ya kisiasa, ni lazima kukemea.

Leo, jambo kubwa zaidi la ma’ruf ni umoja kuzunguka mhimili wa Uongozi wa Mapinduzi na kulinda Mfumo huu wa Kiislamu.
Ni lazima kuwatambua maadui na mipango yao, kwani njia muhimu zaidi ya kukabiliana na adui ni kuzuia mgawanyiko.

Mwisho, ninahisi ni wajibu wangu kuwashukuru kwa dhati wote walioandaa mkutano huu wa kiroho, na naomba mafanikio na tawfiki kwa wote kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha