Washiriki wa Sherehe hiyo pia walimuenzi Mtume Mtukufu (S.A.W.W) kwa heshima kubwa, na walieleza haja ya mshikamano, maelewano, na Umoja wa Umma wa Kiislamu katika kukabiliana na changamoto zinazoukabili ulimwengu wa Kiislamu kwa ujumla.
ASHURA ni siku ya kumi ya mwezi mtukufu wa Muharram. Katika siku hii ya Ashura mjukuu wa Mtume yaani Imam Hussain (as) aliuawa katika tambarare za mji wa Karbala baada ya kusimama kidete dhidi ya mtawala dhalimu wa wakati ule, Yazid bin Muawiya, akatoa fundisho la kukataa kumpigia magoti mdhalimu huyo, ndipo akajitolea maisha yake, akauawa ili kunusuru ubinaadamu , utu pamoja na kupigania uislamu.