Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Katika mahojiano maalum na Redio ya Iqra FM leo, Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Kenya, Mheshimiwa Dkt. Ali Gholampour, alizungumza kuhusu:
1_Kukuza uhusiano wa pande mbili kati ya Iran na Kenya
2_Uvunjifu wa amani na uchokozi wa hivi karibuni uliofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran
3_Mauaji ya halaiki yanayoendelea huko Gaza
4_Uhalifu wa Marekani na Israel dhidi ya binadamu
5_Haja ya dharura ya umoja wa Waislamu Duniani
Aidha, aligusia kuhusu:
6_Tume ya Pamoja ya Iran na Kenya
7_Fursa za masomo na ufadhili wa elimu kwa Wakenya nchini Iran
8_Ushirikiano wa kitamaduni kati ya mataifa haya mawili rafiki.
Mahojiano hayo yalitoa taswira ya msimamo wa Iran kuhusu masuala ya kimataifa na njia za kuimarisha ushirikiano na nchi za Kiafrika.
Your Comment