Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Abbas Sarout, aliyekuwa mbunge wa zamani wa Bunge la Iraq, amesema kuwa ndani ya muungano huo wa Kishia tayari kumefikiwa makubaliano ya awali juu ya mtu maalumu anayetarajiwa kuchukua wadhifa wa Uwaziri Mkuu.
Sarout amesisitiza kuwa njia iliyo mbele si rahisi, akieleza kuwa Iraq inakabiliwa na changamoto tata za kikanda na kimataifa, sambamba na migogoro mingi ya ndani.
Ameongeza kuwa Waziri Mkuu ajaye anatakiwa kuwa na uwezo mkubwa wa kubadilika (unyumbufu) katika kusimamia migogoro, hususan mgogoro wa kifedha na upungufu wa bajeti, pamoja na kuwa na uwezo wa kukabiliana na shinikizo na majukumu mazito ya awamu mpya ya uongozi.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, muungano wa Mfumo wa Uratibu wa Vyama vya Kishia Iraq unapanga kufanya mkutano muhimu katika nyumba ya Nouri al-Maliki, kiongozi wa muungano wa Dola ya Sheria, kwa lengo la kukamilisha na kuhitimisha maelezo ya mwisho kuhusu uteuzi wa mgombea wa Uwaziri Mkuu wa Iraq.
Your Comment