Ayatollah Musawi alisisitiza kuwa jina “Nasrallah” lina mizizi katika nusra ya Mwenyezi Mungu, na historia ya mapambano imethibitisha kuwa licha ya gharama kubwa, irada ya umma kuendeleza njia ya mashahidi na kufikia ushindi haitadhoofika kamwe.
Kiongozi wa Baraza la Maulamaa wa Kishia Pakistan ameeleza kuwa:
> “Hadi pale ambapo suala la Kashmir halitatatuliwa kwa mujibu wa maazimio ya Umoja wa Mataifa, kufanikisha amani ya kudumu katika ukanda huu kutabaki kuwa ni ndoto ya mchana (serabu) tu.”