11 Novemba 2025 - 19:04
Sayyid Isa Tabatabaei alitia roho ya mapambano ndani ya jamii ya Kishia / Mradi bado kuna uvamizi, basi mapambano yataendelea kuishi

Kaimu balozi wa zamani wa Ofisi ya Utamaduni wa Iran nchini Lebanon na mshauri wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) amesema: “Iwapo Imam Musa Sadr ndiye aliyeweka misingi ya taasisi za kijamii na kitamaduni za Waislamu wa Kishia nchini Lebanon, basi Sayyid Isa Tabatabaei ndiye aliyepulizia roho ya mapambano ndani ya jamii hiyo na kuifanya roho ya mapambano iwe sehemu ya utambulisho wao.” Kutokana na juhudi zake, harakati ya mapambano ya kisasa nchini Lebanon ilizaliwa — mapambano yaliyofikia kilele chake katika kuunga mkono dhana ya Palestina.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-- hafla ya uzinduzi wa filamu ya “Wakili” ambayo inaelezea historia ya mapambano nchini Lebanon na nafasi muhimu ya Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Isa Tabatabaei — mwakilishi wa Imam Khomeini (r.a) na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Lebanon — ilifanyika siku ya Jumatano katika Husseiniyya ya Sanaa.

Katika hafla hiyo, Muhammad Mahdi Shariatmadar, aliyewahi kuwa kaimu balozi wa Ofisi ya Utamaduni ya Iran nchini Lebanon, alimuelezea mwanachuoni huyo shujaa kuwa ni mtu wa kipekee, aliyepitia majeraha kutoka kwa adui lakini pia aliyekuwa msingi wa njia ya mapambano.

Sifa na nafasi ya Sayyid Isa Tabatabaei

Shariatmadar alianza kwa kushukuru Husseiniyya ya Sanaa na Tamasha la Ammar kwa kuandaa hafla hiyo akisema: “Ninawashukuru kwa mara ya pili kwa kumtukuza mtu huyu adimu. Mara ya kwanza walimuenzi katika Tamasha la Ammar, na sasa tena wanamkumbuka mtu aliyepata majeraha — si tu kutokana na adui bali pia kutokana na magumu ya njia yake ya jihadi.”

Alibainisha kuwa kama kazi inavyoonyesha ubora wa mtunzi wake, ndivyo mafanikio ya Sayyid Isa yanavyoonyesha undani wa nafsi yake. Ingawa filamu ‘Wakili’ ni kazi yenye thamani, haijaweza kuonyesha upeo wa utu wa Tabatabaei, kwa sababu yeye ni zaidi ya filamu.

Historia ya mapambano nchini Lebanon

Akiweka muktadha wa kihistoria, Shariatmadar alisema: “Kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, kulikuwa na wanazuoni watatu wakubwa walioweka msingi wa mapambano nchini Lebanon: Imam Musa Sadr, Sayyid Muhammad Hussein Fadlallah, na Sheikh Muhammad Mahdi Shamsuddin.
Baada ya mapinduzi, wanazuoni na wasomi kutoka Iran kama Imam Musa Sadr, Shahidi Mustafa Chamran, Ayatollah Akhtari, marehemu Mottashami-Pour na marehemu Hussein Sheikh al-Islam waliendeleza njia hiyo. Lakini miongoni mwao wote, Sayyid Isa Tabatabaei alikuwa na nafasi ya kipekee.”

Alisisitiza: “Iwapo Imam Musa Sadr ndiye aliyeweka taasisi za kijamii na kitamaduni za Kishia nchini Lebanon, basi Sayyid Isa Tabatabaei ndiye aliyepulizia roho ya mapambano katika mwili wa jamii ya Kishia na akaifanya roho ya mapambano kuwa sehemu ya utambulisho wao. Kutokana na juhudi zake, mapambano ya kisasa ya Lebanon yalizaliwa, na baadaye yakafikia kilele katika kuunga mkono dhana ya Palestina.”

Maisha yenye misukosuko

Shariatmadar aliendelea kuelezea maisha ya Tabatabaei akisema: “Sayyid Isa alizaliwa yatima, akapoteza mama yake akiwa mtoto, na akaishi miaka mingi akiwa mbali na nyumbani. Kutoka Najaf hadi Damghan, Qom na Kermanshah, kisha kuelekea Iraq na Lebanon, alipitia maisha yenye changamoto nyingi. Lakini kutoka katika uhamisho huo, alitokea mtu aliyesaidia kuunda mustakabali wa Waislamu wa Kishia nchini Lebanon, harakati ya mapambano ya Kiislamu, na mwelekeo wa umoja wa Kiislamu.”

Aliongeza kuwa: “Sayyid Isa alipata elimu yake ya kidini katika Damghan, Qom na Kermanshah, na alivalishwa kanzu ya ualimamu na Shahidi Ashrafi Isfahani. Alisema kipindi hicho ndicho kilichokuwa bora zaidi maishani mwake. Huko Kermanshah alikutana na Fadhaa’iyin-e Islam na kusoma kitabu cha Kashf al-Asrar cha Imam Khomeini (r.a) — ambacho kilikuwa kiunganishi chake na fikra za uongozi wa Waliyyul-Amr na siasa za Kiislamu.”

Mchango mkubwa kwa jamii ya mapambano

Shariatmadar alisema kuwa Sayyid Isa alianzisha karibu taasisi zote za misaada, kitamaduni, kidini na kiafya katika jamii ya mapambano ya Kishia nchini Lebanon:

  • Kamati ya Misaada (Komite-ye Emdad)
  • Shirika la Mashahidi (Bonyad-e Shahid)
  • Taasisi ya Majeruhi wa Vita
  • Mfuko wa Mikopo Bila Riba (Qardhul-Hasan)
  • Jihadi ya Ujenzi (Jihad Sazandegi)
  • Taasis ya Kowsar
  • Vituo 40 vya Utamaduni vya Imam Khomeini katika miji na vijiji
  • Hospitali ya Rasul A’zam huko Beirut
  • Hospitali ya Sheikh Raghib Harb huko Nabatieh
  • Hawza ya Imam Khomeini huko Baalbek
  • Kaburi la Bibi Khawlah (a.s) huko Baalbek
  • Muungano wa Wanazuoni wa Kiislamu (Tajammu’ Ulama al-Muslimin)
  • Televisheni ya Al-Manar
  • Shule za Misaada (Madaris al-Imdad) 
  • “Taasisi hizi leo ni nguzo kuu za jamii ya mapambano ya Lebanon,” alisema.

Aliongeza kuwa: “Sayyid Isa aliwakabidhi taasisi hizi zote kwa Hizbullah, jambo linalodhihirisha kiwango chake cha ikhlasi na kutojali madaraka wala mali. Ni wachache wanaoweza kufanya hivyo bila kutaka faida binafsi.”

Ustahimilivu wa kiroho

Akizungumzia upande wa kiroho wa mwanazuoni huyo, Shariatmadar alisema: “Safari yake ya kwanza ya Hija aliifanya kwa niyya ya Bibi Fatimah Zahra (a.s). Alikuwa na uhusiano wa karibu sana na Qur’ani — alikuwa akisoma angalau sehemu mbili (juzuu) kila siku, na wakati mwingine katika mwezi wa Ramadhani alikuwa akimaliza Qur’ani nzima kwa siku moja.”

Aliongeza kuwa Sayyid Hassan Nasrallah mara nyingi amemsifu Sayyid Isa kwa ikhlasi na mapenzi yake ya dhati kwa watu wa Lebanon, familia za mashahidi, na wapiganaji wa mapambano.

“Mradi kuna uvamizi, mapambano yataendelea”

Shariatmadar akihitimisha hotuba yake alisema: “Katika filamu hii kuna swali: je, Israel inaweza kumaliza historia ya mapambano?
Jibu ni hapana - mradi bado kuna uvamizi, mapambano yataendelea kuishi.
Mapambano si bunduki na makombora tu, bali ni roho iliyomo ndani ya waumini wanaotambua.
Hata katika lugha ya sheria za kimataifa, haki ya kujitetea kupitia mapambano inatambuliwa.”

Na akaongeza: “Sayyid Isa Tabatabaei hakuwa mjenga majengo tu, bali alikuwa mjenga utamaduni wa mapambano. Alikuwa na imani kwamba ‘tunaweza kusimama, na tunapaswa kusimama.’”

Shariatmadar alihitimisha kwa kunukuu maneno ya Sayyid Hassan Nasrallah: “Tunapomzungumzia Sayyid Isa, hatuwezi kamwe kutoa hata sehemu ndogo ya haki yake. Haki yake juu yetu, juu ya watu na juu ya njia ya mapambano, ni haki kubwa na ya kudumu milele.”

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha