6 Agosti 2025 - 00:34
Likizo ya Wiki Moja katika Mkoa wa Najaf Al-Ashraf kwa Ajili ya Kuwakaribisha Mazuwwari wa Arubaini

Baraza la Mkoa wa Najaf Al-Ashraf limetangaza likizo ya wiki moja kwa ofisi zote za serikali katika mkoa huo, ili kuwezesha ushiriki wa wananchi katika maadhimisho ya Arubaini ya Imam Hussein (a.s) na kutoa huduma bora kwa maelfu ya mahujaji wanaoelekea Najaf Ashraf.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Baraza la Mkoa wa Najaf Al_Ashraf limetoa taarifa rasmi leo hii Jumanne, likisema kuwa likizo ya Wiki Moja kwa ajili ya kuwakaribisha Mazuwwari itaanza siku ya Alhamisi, tarehe 16 Mfunguo Nne (Agosti), hadi tarehe 27 mwezi huo.

Hata hivyo, taasisi za usalama na huduma za msingi hazitahusishwa na likizo hiyo.

Hussein Al-Isawi, Mwenyekiti wa Baraza la Mkoa wa Najaf Ashraf, amesema kuwa:
"Uamuzi huu umechukuliwa ili kutoa nafasi kwa wakaazi wa Najaf kushiriki kikamilifu katika ibada za Arubaini na pia kuwezesha utoaji huduma kwa maelfu ya wageni wanaokuja kushiriki maombolezo ya Arubaini ya Imam Hussein (a.s)."

Maadhimisho ya Arubaini hujumuisha mamilioni ya mahujaji kutoka Iraq na sehemu mbalimbali duniani, na Najaf Ashraf ni moja ya vituo vikuu vya maandalizi ya matembezi ya kuelekea Karbala.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha