Hii ni kwa mara nyingine tena, Sauti ya Tanzania kuinuliwa Katika Haram Tukufu ya Imam Ali (A.S), katika Mji Mtukufu wa Najaf Al-Ashraf Nchini Iraq, kupitia Mwanafunzi huyu Mpenzi wa Mtume Muhammad (saww) na Aali zake Muhammad (Amani iwe juu yao).
Baraza la Mkoa wa Najaf Al-Ashraf limetangaza likizo ya wiki moja kwa ofisi zote za serikali katika mkoa huo, ili kuwezesha ushiriki wa wananchi katika maadhimisho ya Arubaini ya Imam Hussein (a.s) na kutoa huduma bora kwa maelfu ya mahujaji wanaoelekea Najaf Ashraf.