Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Sheikh Mustafa Khatibu Nkonga, Mwanafunzi wa Kitanzania anayesoma nchini Iraq, amepata fursa adhimu na ya kipekee ya kusoma Maatam ya Maombolezo ya Arubaini ya Imam Hussein (a.s) - Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) - katika Mimbari ya Haram Tukufu ya Imam Ali bin Abi Talib (a.s), iliyopo katika Mji Mtukufu wa Najaf Al-Ashraf.
Hii ni heshima kubwa si tu kwake binafsi, bali pia kwa Tanzania na Waislamu wote Wapenzi wa Ahlul-Bayt (as) Waliopo katika ukaenda wa Afrika Mashariki, kuwakilishwa katika Jukwaa Takatifu la Ahlul-Bayt (a.s).
Kwa mara nyingine tena, Sauti ya Tanzania imeinuliwa katika anga la Najaf Al-Ashraf kupitia Mwanafunzi huyu Mchaji Mungu, na Mpenzi wa Mtume Muhammad (S.A.W.W) na Aali zake Watoharifu (A.S).
Your Comment