Najaf
-
Iraq Yaandaa Mazishi ya Kihistoria ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatollah Sayyid Ali Khamenei (ra)
Marasimu ya kihistoria ya mazishi ya mwili mtukufu wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Hussein Khamenei, pamoja na mashahidi wa familia yake, yanafanyika leo nchini Iraq kwa ushiriki wa maelfu ya waombolezaji.
-
Mwanasiasa wa Pakistan: Kiongozi Shahidi Imam Khamenei Aliifanya Iran Kuwa Taifa la Mapambano na Kuunganisha Umma Dhidi ya Uzayuni
Naibu Kiongozi wa Jamaat-e-Islami Pakistan, Liaqat Baloch, amesema Kiongozi Shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei (r.a.) aliiongoza Iran kwa misingi ya Mapinduzi ya Kiislamu na kuifanya kuwa taifa la mapambano, huku akisisitiza umoja wa Umma wa Kiislamu na uungaji mkono wa kudumu kwa Palestina.
-
Rais wa Iran Masoud Pezeshkian Awasili Najaf Kushiriki Mazishi ya Kiongozi Shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Dkt. Masoud Pezeshkian, amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Najaf nchini Iraq kwa ajili ya kushiriki katika mazishi ya Kiongozi Shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, ambapo alipokelewa na Waziri Mkuu wa Iraq pamoja na viongozi wengine waandamizi wa nchi hiyo.
-
Mwakilishi wa Ayatollah Sistani Ataongoza Swala ya Janaza ya Kiongozi Shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei katika Haram ya Imam Hussein (a.s)
Uongozi wa Ataba Tukufu ya Imam Hussein (a.s.) umetangaza kukamilisha maandalizi yote ya kupokea msafara wa mazishi ya Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, huku swala ya janaza ikitarajiwa kuongozwa na mwakilishi wa Marjaa Mkuu Ayatullah Sayyid Ali al-Sistani, Sheikh Abdul Mahdi al-Karbala'i.
-
Marasimu ya Kumuaga Shahidi Sayyid Ali Khamenei yakamilika Qom, Mazishi Yataendelea Katika Miji ya Najaf na Karbala
Marasimu ya kihistoria ya kumuaga Shahidi Ayatollah Shahidi Sayyid Ali Khamenei yamehitimishwa katika Mji mji Mtakatifu wa Qom, huku mwili wake ukitarajiwa kuwasili Najaf usiku wa Kuamkia Jumatano kabla ya kupelekwa Najaf na Karbala kwa ajili ya mazishi
-
Mwanafunzi wa Kitanzania Apewa Heshima ya Kusoma Maatam ya Arubaini ya Imam Hussein (A.S) Katika Haram ya Imam Ali (A.S), Najaf Al-Ashraf
Hii ni kwa mara nyingine tena, Sauti ya Tanzania kuinuliwa Katika Haram Tukufu ya Imam Ali (A.S), katika Mji Mtukufu wa Najaf Al-Ashraf Nchini Iraq, kupitia Mwanafunzi huyu Mpenzi wa Mtume Muhammad (saww) na Aali zake Muhammad (Amani iwe juu yao).