Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Katika safu ya matembezi ya Arbaeen kutoka Najaf hadi Karbala, kwenye nguzo namba 379, kuna Maukib maalumu inayoendeshwa na ndugu wanafunzi wa kidini kutoka Bara la Afrika.
Ndugu hawa wapo katika huduma za kiutamaduni na kidini, wakitoa huduma kwa lugha kadhaa tofauti ili kuwahudumia mazuwaru wa kila taifa.
Insha Allah, kutakuwepo na fursa ya kufanya mkutano wa mazungumzo ya vijana wa Iran na Afrika utakaofanyika katika eneo hili, na hili bila shaka ni jambo zuri na jema na lenye kuleta furaha kubwa kwa kuwakutanisha ndugu na jamaa wapenzi wa Ahlulbayt (as).
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kwa moyo mkunjufu, linatoa pongezi na shukrani kwa juhudi zenu nzuri kwa kuandaa Maukib hii.
Na Maneno yetu Daima ni haya:
《 يا ليتنا كنا معك يا أباعبدالله، فنفوز فوزا عظيما 》
“Ewe Aba Abdillah!, Laiti tungelikuwa pamoja nawe, basi tungelipata kufuzu kukubwa (na ushindi mkubwa).”
Your Comment