"Kwa juhudi za Imam na Mapinduzi, jina la Ahlul Bayt (a.s) limejulikana na kutambulika kote duniani. Sababu kuu ya uadui wote wa naadui dhidi ya IRAN, unatokana na IRAN na Jamhuri ya Kiislamu kuzingatia na kufuatilia zaidi mafundisho ya Ahlul-Bayt (a.s). Kuanzia vita vya miaka minane hadi fitina ya Daesh na hata uvamizi huu wa utawala wa Kizayuni ni kwa sababu ya imani ya dhati ya Taifa la Iran na uvumilivu wa Mashia."
Hii ni kwa mara nyingine tena, Sauti ya Tanzania kuinuliwa Katika Haram Tukufu ya Imam Ali (A.S), katika Mji Mtukufu wa Najaf Al-Ashraf Nchini Iraq, kupitia Mwanafunzi huyu Mpenzi wa Mtume Muhammad (saww) na Aali zake Muhammad (Amani iwe juu yao).