15 Juni 2025 - 16:21
Marasimu ya Mazishi ya Miili Mitukufu ya Mashahidi wa Walinzi na Watetezi wa ngazi za juu wa Iran ya Kiislamu itafanyika

Baraza la Uratibu wa Propaganda za Kiislamu limetangaza katika taarifa yake kwamba, hafla ya mazishi ya miili mitukufu ya mashahidi wa ngazi za juu ambao ni walinzi na watetezi wa Iran ya Kiislamu itafanyika Siku ya Jumanne, tarehe 17 Juni, 2025, saa 8:00 Asubuhi katika Medani ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Tehran.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul Bayt (as) - ABNA-, Baraza la Uratibu wa Propaganda za Kiislamu limetangaza katika taarifa yake kwamba, hafla ya mazishi na maziko ya miili mitukufu ya Mashahidi wa Jamhuri ya Kiislamu itafanyika Jumanne tarehe 17 Juni 2025, saa 8:00 Asubuhi katika Medani ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Tehran.

Nakala kamili ya taarifa ni kama ifuatavyo:

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

إِنَّ الَّذِینَ قَالُوا رَبُّنَا اللَّهُ ثُمَّ اسْتَقَامُوا تَتَنَزَّلُ عَلَیْهِمُ الْمَلَائِکَةُ أَلَّا تَخَافُوا وَلَا تَحْزَنُوا وَأَبْشِرُوا بِالْجَنَّةِ الَّتِی کُنْتُمْ تُوعَدُونَ (فصلت:۳۰ )

Hakika wale walio sema: Mola wetu ni Mwenyezi Mungu, kisha wakawa na msimamo sawa , Malaika watawateremkia na kuwaambia: “Msiogope wala msihuzunike, na pokeeni bishara ya Pepo mliyokuwa mkiahidiwa. (Fussilat: 30).

Taifa adhimu na lenye kulea Mashahidi la Iran ya Kiislamu,

Kufuatia hujuma na mashambulio ya kinyama ya utawala wa Kizayuni katika ardhi takatifu ya Jamhuri ya Kiislamu, kundi la makamanda shupavu wa jeshi la nchi hiyo, wanasayansi mashuhuri wa nyuklia na watu wasio na hatia wakiwemo wanawake na watoto waliodhulumiwa wameuliwa na kufanikiwa kupata sharafu ya Shahada na daraja la juu kabisa. Kuchanganywa damu safi ya makundi mbalimbali ya watu na damu ya mashahidi wa nyuklia, maendeleo ya kisayansi na makamanda wa kijeshi wanaowajibika kwa mamlaka na madaraka ya nchi kulikuwa na maana kubwa sana katika kudhihirisha uadui wa maadui kwa maendeleo na mamlaka ya Iran.

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi linautaarifu umma kwa ujumla kwamba hafla za mazishi ya miili mitakatifu ya mashahidi hao wa ngazi za juu zitafanyika Jumanne tarehe 17 Juni 2025, saa 8:00 Asubuhi kutoka Medani ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Tehran.

Baraza la Uratibu wa Propaganda za Kiislamu linawaalika wananchi wote wa taifa kubwa la Iran kuhudhuria kwa shauku katika hafla hii adhimu, kuhuisha dhamira yao ya kutimiza malengo ya Mapinduzi ya Kiislamu na kuheshimu kumbukumbu za Mashahidi, na kwa mara nyingine tena kuonesha azma yao thabiti ya kuilinda nchi na kuwapinga kikamilifu maadui, na kuunga mkono kikamilifu oparesheni za jeshi la wanajeshi shupavu la Iran dhidi ya utawala ghasibu wa Kizayuni.

Ahadi yetu: Jumanne, Juni 17, 2025, 8:00 Asubuhi, katika medani ya Mapinduzi, Tehran.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha