Kwa mujibu wa Politico, hofu kuu ya Washington kuhusu kushambulia Iran ni kupungua kwa akiba ya silaha na uwezekano wa vifo vya wanajeshi wa Marekani, jambo linaloifanya ipime kwa makini kabla ya kuchukua hatua ya kijeshi.
Baraza la Uratibu wa Propaganda za Kiislamu limetangaza katika taarifa yake kwamba, hafla ya mazishi ya miili mitukufu ya mashahidi wa ngazi za juu ambao ni walinzi na watetezi wa Iran ya Kiislamu itafanyika Siku ya Jumanne, tarehe 17 Juni, 2025, saa 8:00 Asubuhi katika Medani ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Tehran.