13 Septemba 2025 - 16:23
Idadi ya Mashahidi wa Gaza yafikia 64,803

Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa jumla ya mashahidi katika eneo hilo imefikia watu 64,803.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Wizara ya Afya ya Palestina leo Jumamosi imesema kuwa ndani ya masaa 24 yaliyopita, Mashahidi 47 na Majeruhi 205 wapya wamefikishwa katika Hospitali za Gaza.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari Ma’an, tangu kuanza kwa vita vya mauaji ya kimbari vilivyoanzishwa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza tarehe 7 Oktoba 2023 hadi sasa, jumla ya mashahidi imepanda hadi 64,803 na majeruhi kufikia 164,264.

Aidha, kuanzia tarehe 18 Machi 2025 hadi leo, kumerekodiwa mashahidi 12,253 na majeruhi 52,223.

Miongoni mwa wahanga waliokuwa wakisubiri kupokea misaada ya chakula, ndani ya masaa 24 yaliyopita, mashahidi 5 na majeruhi 26 wamefikishwa hospitalini, na kufanya idadi ya mashahidi wa sehemu hii kufikia 2,484, huku majeruhi wakizidi 18,117.

Vilevile, watu 7 wakiwemo watoto 2 wamefariki kutokana na njaa na utapiamlo katika hospitali, na kufanya jumla ya wahanga wa utapiamlo kufikia 420, wakiwemo watoto 145.

Tangu kutangazwa kwa hali ya njaa kali huko Gaza, kesi 142 za vifo kutokana na utapiamlo zimerekodiwa, ambapo 30 kati yao walikuwa watoto.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha