abna
-
Mtindo wa Maisha wa Fatima (a.s) na Kauli “Jirani Kwanza Kisha Nyumba”: Kigezo cha Kiungu Kukabiliana na Ubinafsi wa Kisasa
Katika kuelekea kumbukizi ya kuzaliwa kwa Bibi Fatima Zahra (a.s), kikao cha kisayansi kuhusu “Mtindo wa Maisha wa Fatima na Mafundisho ya al-jār thumma al-dār (Jirani Kwanza Kisha Nyumba)” kiliandaliwa kwa ushirikiano na Shirika la Habari la ABNA, ambapo watafiti walibainisha changamoto za familia katika enzi ya kisasa—hususan mgongano kati ya fikra za kisasa na mwenendo wa kimapokeo. Katika kikao hicho, mfano wa Maisha wa Bibi Zahra (a.s) uliwasilishwa kama muongozo wa kiungu na wa vitendo unaojenga maadili ya kuwajali wengine na kuleta mizani kati ya haki na wajibu ndani ya familia.
-
Mchambuzi wa Kisiasa wa Lebanon:
Mkutano wa Kiuchumi na Wawakilishi wa Israel ni Uongo Mtupu na Vita vya Kisaikolojia / Muqawama Haitaruhusu Aina Yoyote ya Uhalalishaji wa Mahusiano
Katika mazungumzo yake na ABNA, Fadi Boudieh alisema kuwa bila shaka Israel inajaribu kuwapotosha baadhi ya Walebanoni, Waisraeli na hata baadhi ya nchi za Kiarabu, kwa kuwashawishi kuwa imefanikiwa kulazimisha hali mpya ya kiuchumi kwa Lebanon kwa kutumia nguvu, na kwamba chaguo la upinzani (Muqawama) limekwisha.
-
Profesa wa Chuo Kikuu cha Indonesia katika mahojiano na ABNA:
“Iran ni mfano wa kipekee wa maendeleo ya kisayansi na uimara dhidi ya vikwazo – ni lazima mtu aione kwa macho yake”
Amesema kuwa uongo mwingi kuhusu Iran unatolewa na taasisi zinazopingwa na msimamo wa Iran wa kusimama dhidi ya Marekani na Israel. Hata hivyo, baada ya vita vya siku kumi na mbili, wanafikra wengi duniani wamekiri wazi kwamba Iran ndilo taifa pekee lililosimama dhidi ya dhulma kwa njia ya kivitendo, si kwa maneno tu.
-
Idadi ya Mashahidi wa Gaza yafikia 64,803
Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa jumla ya mashahidi katika eneo hilo imefikia watu 64,803.