Brigedia Jenerali Mohammad Baqerzadeh amesema hali ya kiafya ya marubani wa Iran wanaoshikiliwa nchini Qatar ni mbaya sana, akitoa wito kwa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu kupeleka ndege ya matibabu nchini Qatar ili kuhakikisha majeruhi hao wanarejeshwa Iran haraka iwezekanavyo.
Msemaji wa Vikosi vya Ulinzi vya Iran, Brigedia Jenerali Abolfazl Shekarchi, ameonya kuwa Iran haitakaa kimya mbele ya kuendelea kwa mashambulizi ya Israel dhidi ya Lebanon, akilaani mauaji ya raia na ukimya wa baadhi ya mataifa ya Magharibi.