27 Machi 2025 - 23:04
Rekodi nyingine kwa Israeli; Gaza ina watoto wengi waliokatwa viungo katika historia!

Gaza ina idadi kubwa zaidi ya watoto waliokatwa viungo vyao katika historia ya kisasa, huku Israel ikizidisha mzozo wa kibinadamu kwa kukiuka usitishaji vita na mzingiro.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahl al-Bayt (a.s) - Abna -; Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imeripoti jana kwamba Gaza ina "Kundi kubwa zaidi la Watoto waliokatwa viungo katika historia ya kisasa".

Kwa mujibu wa Middle East Eye, mpango wa msaada walemavu wa Shirika la Misaada la Medical Aid "Msaada wa Matibabu kwa Wapalestina" (MAP) lenye Makao yake Makuu nchini Uingereza, Ilitangaza kuwa msaada uliotolewa kwa watoto waliokatwa viungo wakati wa usitishaji mapigano, ulitosheleza 20% tu ya mahitaji.

Mpango huo pia uliongeza kuwa Israel inazuia uingiaji wa vifaa vinavyohitajika kutengenezea viungo vya bandia, ikidai kuwa vifaa hivi vinaweza kutumika kwa madhumuni ya kijeshi.

Vikosi vinavyoikalia Palestina kwa mabavu vya Israel vilianza tena mashambulizi yao huko Gaza mapema Machi 18, na hivyo kuhitimisha usitishaji mapigano ulioanzishwa tangu Januari 19. Wakati wa usitishaji (vita) mapigano, kituo cha pamoja cha operesheni za Misri na Qatar ambacho kilifuatilia utekelezaji wa makubaliano hayo kilirekodi zaidi ya ukiukaji 900 wa usitishaji vita uliofanywa na Israel katika siku 40 kabla ya Israel kuanza tena mashambulizi yake ya mabomu Machi 18.

Ukiukaji huu ulijumuisha operesheni za kijeshi ambazo zilisababisha vifo vya zaidi ya Wapalestina 70. Aidha, Israel ilizuia kuingia kwa misafara ya misaada ya kibinadamu na mahema muhimu kwa ajili ya kuwapokea watu waliokimbia makazi yao huko Gaza baada ya jeshi la Israel kuharibu zaidi ya asilimia 70 ya miundombinu ya Gaza, zikiwemo Nyumba, Shule, Misikiti, Makanisa na Mitaa.

Mashambulizi ya mara kwa mara katika maeneo mbalimbali ya Gaza hadi sasa yamesababisha vifo vya watu 730 na kujeruhi watu 1,367, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Palestina.

Wakati huo huo, serikali ya Benjamin Netanyahu inakataa kuendelea na mazungumzo ya awamu ya pili ya makubaliano ya kusitisha mapigano, huku ikitaka kuwaachia huru wafungwa (mateka) zaidi wa Israel bila kutimiza ahadi za Tel Aviv chini ya makubaliano hayo; Ahadi ambazo ni pamoja na kukomesha mashambulizi makubwa na kujiondoa kabisa kutoka Gaza.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha