20 Agosti 2025 - 16:41
Kuongezeka kwa Idadi ya Mashahidi wa Njaa Gaza hadi 269

Wizara ya Afya ya Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa katika saa 24 zilizopita watu wengine watatu wamepoteza maisha yao kutokana na njaa na ukosefu wa chakula.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Wizara ya Afya ya Gaza imeripoti kufariki kwa watu watatu zaidi katika eneo hilo kutokana na baa la njaa na uhaba wa chakula katika kipindi cha saa 24 zilizopita, na kwa hali hiyo idadi ya mashahidi waliokufa kwa njaa iliyosababishwa na utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wa Palestina imefikia 269, wakiwemo watoto 112.

Habari hii inakuja huku Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya katika Ukanda wa Gaza akitangaza kuwa wavamizi wa Kizayuni wanamuua shahidi mtoto mmoja kila baada ya dakika 40 huko Gaza, na kila siku watoto 28 hupoteza maisha yao kutokana na mashambulizi ya mabomu.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha