Darasa huanza saa moja kabla ya Swala ya Adhuhuri na Alasiri, na baada ya kumalizika, Swala ya Adhuhuri na Alasiri husaliwa kwa pamoja kwa uwepo wa Masheikh na walimu. Washiriki: Ni Wanafunzi wote wa madrasa, pamoja na walimu na wasimamizi wa bweni.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Darasa na warsha hii ya Qur’ani hufanyika kila siku ya Jumanne, chini ya usimamizi wa Mwalimu na Ustadh mashuhuri, Bwana Muhammad Ja‘far.
Vipindi hivi huendeshwa kwa kutumia mbinu ya Tajwīd (usomaji sahihi wa Qur’an), pamoja na mafunzo ya kusoma Qur’an kwa ufasaha, ladha na ustadi wa juu kabisa. Pia kuna kipindi cha maswali na majibu, ambapo kila mwanafunzi atakayetoa jibu sahihi huzawadiwa zawadi maalumu.
Muda wa Programu:

Your Comment