Hali ya sasa ya utawala wa Kizayuni (Israel) kutokana na utegemezi wake mkubwa kwa siasa za Marekani pamoja na changamoto za ndani, imegeuka kuwa moja ya hatua muhimu za kihistoria katika uhusiano wa kimataifa wa utawala huo. Mabadiliko haya yanaweza kusababisha mabadiliko ya kimkakati katika siasa za Israel na namna inavyoshirikiana na jamii ya kimataifa na Wapalestina.
Wizara ya Afya ya Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa katika saa 24 zilizopita watu wengine watatu wamepoteza maisha yao kutokana na njaa na ukosefu wa chakula.