10 Agosti 2025 - 15:23
Magharibi mwa Asia na Mashariki ya Kati | Watu 11 Wauawa na Kujeruhiwa Kutokana na Mlupuko wa Mabomu Yaliyosalia huko Tyre, Lebanon

Watu 11 wa jeshi la Lebanon wameuawa na kujeruhiwa kufuatia mlipuko wa mabomu yaliyosalia kutoka kwenye uvamizi wa awali wa utawala wa Kizayuni kusini mwa Lebanon, tukio ambalo limepelekea viongozi wa juu wa nchi hiyo kutuma salamu za rambirambi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- vyombo vya habari vya Lebanon vimeripoti kuwa mlipuko huo umetokea katika kijiji cha Majdal Zoun, mkoa wa Tyre, kusini mwa Lebanon, wakati wanajeshi wa jeshi la Lebanon walipokuwa wakihifadhi na kulipua mabaki ya mabomu kutoka shambulio la awali la Israel.

Chanzo cha habari nchini Lebanon kimeeleza kuwa eneo hilo hapo awali lililengwa na mashambulio ya anga ya Israel na hakuna mtu aliyekuwa ameingia kwa hofu ya milipuko zaidi, hadi kikosi cha uhandisi cha jeshi la Lebanon kilipoingia, ambapo mlipuko ulitokea.

Kwa mujibu wa Russia Al-Youm, watu sita wamefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa katika tukio hilo, na wote walipelekwa hospitalini. Wanne kati ya waliokufa walikuwa wa Kikosi cha Tano cha Jeshi, na wawili walikuwa wa Kikosi cha Uhandisi.

Rais wa Lebanon, Joseph Aoun, alipokea taarifa ya kina kutoka kwa Kamanda wa Jeshi, Jenerali Rudolf Heikal, kuhusu tukio hilo lililotokea katika eneo la Majdal Zoun - Wadi Zbaki, kaunti ya Tyre. Akiwasilisha rambirambi zake kwa familia za mashujaa hao na jeshi lote, aliongeza kuwa:
"Leo, taifa letu limewapoteza baadhi ya wana wake bora waliotoa maisha yao kwa ajili ya kulinda ardhi na uhuru wa Lebanon. Mashahidi hawa kwa damu zao wameandika maana halisi ya kujitolea na uaminifu, wakithibitisha kuwa jeshi la Lebanon litaendelea kuwa ngao ya taifa na mlinzi mwaminifu wa mipaka yake."

Waziri Mkuu wa Lebanon, Nawaf Salam, katika tamko lake alisema:
"Kwa moyo uliojaa uchungu, tumepokea habari za kuuawa mashujaa wa jeshi la Lebanon waliokuwa wakitimiza wajibu wao wa kitaifa kusini. Taifa lote - Serikali na wananchi - linainama kwa heshima mbele ya kujitolea na damu yao safi, tukikumbuka kuwa jeshi letu ndilo dhamana ya usalama, ngome ya uhuru na mlinzi wa umoja wa taifa pamoja na taasisi zake halali."

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha