14 Agosti 2025 - 12:30
Dkt. Larijani: Sayyid Hassan Nasrallah alikuwa hazina kubwa kwa ulimwengu wa Kiislamu

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, katika ziara yake kwenye eneo la Dahieh Kusini mwa Beirut na kutembelea kaburi la Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, alimueleza kuwa ni hazina kubwa kwa ulimwengu wa Kiislamu na kusisitiza juu ya kuendeleza njia ya muqawama (upinzani wa haki).

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Dkt. Ali Larijani, akiwa pamoja na Mojtaba Amani, Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Lebanon, walitembelea kaburi la Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, kiongozi wa mashahidi wa muqawama, katika eneo la Dahieh Kusini mwa Beirut. Alipokuwepo kaburini, aliweka shada la maua na kusoma Fatiha kwa ajili ya roho yake safi.

Katika eneo hilo kulikuwapo umati mkubwa wa wananchi wa Lebanon na baadhi ya wanazuoni wa dini akiwemo Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Isa Tabatabai, mwana wa shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, Sayyid Jawad Nasrallah pamoja na wanasiasa, viongozi wa vyama, wanaharakati wa kijamii, wanahabari na pia familia za mashahidi wa muqawama wa Kiislamu.

Washiriki walikuwa wameshika bendera za Lebanon na bendera za muqawama, pamoja na picha za Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu na makamanda mashahidi, huku wakipiga kauli mbiu za kuunga mkono Hizbullah, muqawama na Iran.

Katika hotuba yake mbele ya hadhara hiyo, Larijani alisisitiza kuwa: “Sayyid Hassan Nasrallah, kiongozi wa mashahidi wa umma, alikuwa mtu mkubwa na hazina adhimu kwa ulimwengu mzima wa Kiislamu. Sifa iliyomtenganisha na wengine ilikuwa ni kushikamana kwake na misingi na kanuni alizoziamini.”

Dkt. Larijani alieleza kuwa Hizbullah ni harakati hai, yenye kuleta heshima kwa binadamu, chanzo cha fahari kwa umma na chemchemi ya izza na heshima. Aliongeza kuwa harakati iliyoanzishwa na Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah ni ya kudumu milele, na yeye ndiye aliyeweka msingi wa nguvu na uwepo wa Hizbullah.

Akizungumza na wafuasi wa muqawama, alisema: “Uadui wa baadhi yenu unatokana na ushawishi na uthabiti wenu. Ni kweli tumempoteza Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, lakini wanafunzi na watoto wake wa kifikra bado wapo hai.”

Dkt. Larijani: Sayyid Hassan Nasrallah alikuwa hazina kubwa kwa ulimwengu wa Kiislamu

Larijani aliendelea kusema: “Ikiwa mnataka kutembea katika njia ya Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, jukumu lenu ni kudumu na kusimama imara katika muqawama... Njia yenu iko wazi na mwishowe mtashinda.”

Alisisitiza msimamo wa kimsingi wa Iran wa kusimama daima pamoja na watu wa muqawama, na kubainisha kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haiingilii mambo ya ndani ya nchi nyingine.

Dkt. Larijani alimaliza hotuba yake kwa kusisitiza tena kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kuunga mkono harakati zote za muqawama duniani kote.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha