Baraza la Kuratibu Tablighi la Kiislamu limetangaza katika taarifa yake kwamba maadhimisho ya mwaka wa kwanza wa kifo cha shahidi Sayyid Hassan Nasrallah yatafanyika Alhamisi, tarehe 02 Oktoba, 2025, katika nchi nzima, chini ya kauli mbiu kuu “Innā ‘ala al-‘Ahd”. Hafla kuu itafanyika saa 4:00 usiku katika Uwanja wa Ibada wa Imam Hussein (a.s) mjini Teheran.
Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, katika ziara yake kwenye eneo la Dahieh Kusini mwa Beirut na kutembelea kaburi la Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, alimueleza kuwa ni hazina kubwa kwa ulimwengu wa Kiislamu na kusisitiza juu ya kuendeleza njia ya muqawama (upinzani wa haki).