Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (a.s) - Abna - "Abdu al-Malik Badr al-Din al-Houthi", Kiongozi Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen, katika hotuba yake wakati akiwapongeza watu wa Yemen na Umma wa Kiislamu kwa Sikukuu ya Eid-ul-Fitr, aliwashukuru Mujahidina wa Yemen, na kusisitiza jukumu lao la kijeshi katika vikosi vya kijeshi, vikosi vya ulinzi na usalama katika kuihami (na kuilinda) nchi hii.
Kiongozi wa Ansarullah wa Yemen pia alizipongeza familia za Mashahidi, waliojeruhiwa na wafungwa kwa mnasaba wa tukio hili na akasifu na kuthamini uvumilivu wao na kujitolea kwao.
Ameongeza kuwa: Heri watu wa Gaza ambao bado wako imara licha ya mauaji ya kimbari dhidi yao na kuzingirwa (na utawala ghasibu wa kizayuni).
Kiongozi wa Ansarullah ya Yemen amewataka Waislamu kutosahau hali ya Wananchi wa Palestina huko Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan wanaokabiliwa na njaa, mauaji, uharibifu na kuyahama makaazi yao.
Kiongozi wa Ansarullah ameashiria pia mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa na juhudi za Marekani na Israel za kuliangamiza suala la Palestina na kusema: Waislamu wanapaswa kutekeleza wajibu wao mbele ya njama hizo.
Amesisitiza kuwa Wananchi wa Yemen wanaendelea kuiunga mkono kikamilifu Palestina na watasimama daima dhidi ya hujuma za Marekani dhidi ya Yemen.
Kiongozi wa Ansarullah ya Yemen pia ameeleza kuwa mashambulizi ya Marekani dhidi ya Yemen hayawezi kufunika uwezo wa kijeshi wa Yemen na operesheni zake za kuiunga mkono Gaza.
Your Comment