Ayatollah Khamenei amesema kuhusu misimamo ya vitisho ya hivi karibuni ya Marekani: Kwanza, iwapo uovu utafanywa kutoka nje, jambo ambalo bila shaka halina uwezekano mkubwa, kwa hakika watajibiwa kwa kupigwa kwa pigo kali , na pili, ikiwa adui anafikiria kuzusha mpasuko (fitna) kwa ndani, kama ilivyokuwa katika baadhi ya miaka ya nyuma, Taifa litatoa jibu kali kwa waasi (wapenzi wa fitna) kama ilivyokuwa kwa miaka hiyo.
Akitoa salamu za pongezi za Eid al-Fitr, Sayyid Abdul Malik al-Houthi alisema: "Watu wa Gaza hawakufunga tu Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, bali pia walipata heshima ya Jihadi na Upinzani (Muqawamah) dhidi ya wavamizi."