30 Machi 2025 - 21:48
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania awatangazia Waislamu wa Tanzania kuonekana kwa Mwezi

Natumia fursa hii kuthibitisha kuwa Mwezi umeonekana, na Kesho Jumatatu ni Siku ya Eidul - Fitri

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA -; Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mheshimiwa Dr. Abubakar Zubair bin Ali Mbwana, amewatangazia rasmi Waislamu nchini Tanzania kuonekana kwa Mwezi akisema kuwa Mwezi wa Shawwal umeandama na kuonekana maeneo mbalimbali ndani ya Tanzania na nchi jirani ya Kenya, akaongeza:

Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania awatangazia Waislamu wa Tanzania kuonekana kwa Mwezi

Natumia fursa hii kuthibitisha kuwa Kesho Siku ya Jumatatu ni Eidul _ Fitr.

Kwa minajili hiyo, amewapongeza Waislamu wote kwa Mnasaba wa Eid Al_Fitr na kuwatakia Sala Njema ya Eid na Sikukuu Njema ya Eid, sambamba na kuwaalika Waislamu wote katika Baraza la Eid litakalofanyika mida ya jioni katika Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC), ambapo Mgeni Rasmi atakuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha