Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Inaripotiwa kuwa Wanasayansi wa China wametengeneza aina mpya ya bomu lenye nguvu kubwa lisilo la nyuklia. Badala ya kutumia mionzi ya atomiki, bomu hili hutumia Hidrojeni (Hydrogen) pamoja na aina maalum ya Magnesiamu (Magnesium) ili kuunda mpira wa moto wenye joto kali unaodumu kwa muda mrefu.
Mpira huo wa moto unaweza kufikia zaidi ya nyuzi joto 1,000°C na kudumu kwa zaidi ya sekunde mbili - hii ikiwa ni mara 15 zaidi ya muda wa mlipuko wa kawaida wa TNT.
Athari hii ya "tochi ya moto" imelenga kusababisha uharibifu mkubwa kwa joto, ikiwa ni pamoja na kuyeyusha metali ngumu kama alumini, badala ya kutegemea mshtuko mkubwa wa mlipuko.
Habari njema ni kuwa, kwa kuwa bomu hili si la nyuklia, halitoi mionzi yoyote hatari ya sumaku au ya miale ya nyuklia. Teknolojia hii mpya inaweza kubadilisha matumizi ya silaha za nguvu zisizo za nyuklia katika siku zijazo.
Your Comment