13 Oktoba 2025 - 11:16
Mwandishi wa Kizayuni: Hamas bado ipo hai

"Wapiganaji wa Hamas wameonekana hadharani wakiwa wamevaa sare za kijeshi, jambo linalotoa ujumbe wazi kwa wale wote waliodhani kuwa vita vya miaka miwili vya Israel dhidi ya Hamas viliiangamiza, kwamba dhana hiyo imekuwa si sahihi, kwani Hamas imerejea tena kwa nguvu kwenye uwanja wa mapambano".

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Tzvi Yehzkeli, Mwandishi wa habari wa Kizayuni, ametangaza kuwa Hamas imerejea mitaani na imepata tena udhibiti wake, na kwamba si tu imeanza mchakato wa kuwarejesha mateka, bali pia inapambana na machafuko yaliyokuwepo.

Amesema kuwa wapiganaji wa Hamas wameonekana hadharani wakiwa wamevaa sare za kijeshi, jambo linalotoa ujumbe wazi kwa wale wote waliodhani kuwa vita vya miaka miwili vya Israel dhidi ya Hamas viliiangamiza, kwamba dhana hiyo imekuwa si sahihi, kwani Hamas imerejea tena kwa nguvu kwenye uwanja wa mapambano.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha