"Wapiganaji wa Hamas wameonekana hadharani wakiwa wamevaa sare za kijeshi, jambo linalotoa ujumbe wazi kwa wale wote waliodhani kuwa vita vya miaka miwili vya Israel dhidi ya Hamas viliiangamiza, kwamba dhana hiyo imekuwa si sahihi, kwani Hamas imerejea tena kwa nguvu kwenye uwanja wa mapambano".
Shirika la televisheni la Kizayuni Channel 12 limekiri kwamba: “Hamas, katika kipindi cha miaka miwili migumu sana ikiwemo vita ya hivi karibuni, imeonyesha ujasiri na haijashindwa. Lengo kuu la Israel katika vita - yaani ‘kuishinda Hamas’ - halijafanikiwa.”