Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Sayyid Abdulmalik Badruddin al-Houthi, Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen, katika hotuba yake ya leo (Alhamisi: 21 -08- 2025) amelaani ukimya na kutochukua hatua kwa mataifa ya Kiislamu kuhusiana na kile alichokiita “Mauaji ya halaiki ya utawala wa Kizayuni huko Gaza.”
Katika hotuba yake, al-Houthi alieleza kwa masikitiko na ghadhabu hali ya “kutochukua hatua” kwa Waislamu zaidi ya bilioni mbili duniani, akisema kuwa ukimya huo ni “aibu na fedheha” inayoweza kuleta madhara si tu kwa Palestina, bali pia kwa ulimwengu mzima wa Kiislamu.
Ukosoaji kwa Saudi na Misri
Al-Houthi alishutumu vikali baadhi ya serikali za Kiarabu, hasa Saudi Arabia na Misri, akizituhumu kwa ushirikiano wa moja kwa moja na Tel Aviv. Alitaja mkataba wa gesi wa Misri na Israel kuwa ni “janga na msaada wa wazi kwa adui.”
Alisema kuwa fedha hizo kubwa zingetumika ndani ya Misri kwa uwekezaji wa kitaifa au kuagiza kutoka kwa nchi za Kiislamu badala ya kushirikiana na utawala wa Kizayuni.
Aidha, alifichua taarifa kuhusu meli ya Kisaudi iliyoshikiliwa katika moja ya bandari za Italia, ambayo kwa mujibu wa maelezo yake ilikuwa imebeba silaha kwa ajili ya Israel. Alilaani kitendo hicho akisema: “Huu siyo usafirishaji wa kawaida wa silaha tu, bali ni msaada wa kijeshi kwa Israel. Saudi yenye utajiri mkubwa haipaswi kujishusha hadhi na kuwa kama ‘mpagazi wa kukodishwa’ wa adui.”
Kuhusu Mipango ya Utawala wa Kizayuni
Kiongozi huyo wa Ansarullah pia alionyesha mshangao kuhusu mipango ya Waziri Mkuu wa Israel ya kupanua ardhi na kuunda kile kinachoitwa “Israel Kubwa.” Alisema: “Wakati adui anachukua hatua za kivitendo, nchi nyingi za Kiarabu zinabaki kutoa ‘taarifa za karatasi’ bila kuchukua hatua za dhati.”
Uungaji Mkono kwa Wapinzani wa Upinzani
Al-Houthi aliendelea kueleza kuwa baadhi ya serikali za Kiarabu zimekuwa zikitaka makundi ya mapambano kama Hamas huko Gaza na vikosi vya upinzani nchini Lebanon vya silaha, jambo aliloliita kuwa ni msaada wa moja kwa moja kwa Israel.
Alisisitiza kuwa ukimya na kutochukua hatua kwa serikali na taasisi za Kiislamu si jambo la bahati mbaya au udhaifu, bali ni maamuzi ya kisiasa.
Ujumbe kutoka Gaza
Katika hotuba yake, al-Houthi pia alisoma ujumbe wa mmoja wa wapiganaji wa Kipalestina walioko katika mapigano ya Khan Yunis, ambaye aliwaambia Waislamu:
“Sisi ni hoja kwa ajili yenu, sio nyinyi muwe hoja dhidi yetu. Mwenyezi Mungu hatowasamehe wale waliokosa kuchukua hatua.”
Kwa mujibu wa al-Houthi, ujumbe huu unaonyesha roho ya wapiganaji wa Gaza na ni kilio cha kupinga kupuuzwa na ulimwengu wa Kiislamu.
Mwisho wa hotuba yake, al-Houthi alisema kuwa hali ya Umma wa Kiislamu kwa sasa ni mbaya, akasisitiza haja ya kusema ukweli kwa uwazi, kuchukua misimamo ya wazi na hatua za kivitendo dhidi ya kile alichokiita “tishio kwa umma mzima wa Kiislamu.”
Your Comment