Watu wa Yemen katika kumbukumbu ya miaka 11 ya ushindi wa Mapinduzi yao wanapanga kufanya maadhimisho ya kumbukumbu ya Sayyid wa Muqawama, kwa kuwa uhusiano wa Sayyid Muqawama na wananchi pamoja na viongozi wa Yemen ulikuwa ni uhusiano wa pande mbili uliojaa mapenzi na heshima.
Kiongozi wa Ansarullah wa Yemen, akifichua ukubwa wa mauaji ya kimbari na uharibifu wa miundombinu huko Gaza, ametaja pia mipango ya upanuzi ya utawala wa Kizayuni katika eneo la kikanda, ikiwemo Lebanon, Syria na uvamizi wa hivi karibuni dhidi ya Qatar.
Ameitaja Marekani kuwa mshirika katika uhalifu huu na kusisitiza kuendelea kwa mapambano na mshikamano wa Kiislamu katika kukabiliana na uchokozi huu.
Katika hotuba yake, al-Houthi alieleza kwa masikitiko na ghadhabu hali ya “kutochukua hatua” kwa Waislamu zaidi ya bilioni mbili duniani, akisema kuwa ukimya huo ni “aibu na fedheha” inayoweza kuleta madhara si tu kwa Palestina, bali pia kwa ulimwengu mzima wa Kiislamu.