Katibu Mkuu wa Baraza la Maimamu wa Kishia nchini Pakistan, Hujjatul-Islam Shabir Hassan Meesami, amelielezea hatua ya Serikali ya Punjab ya kuwashughulikia kwa nguvu waombolezaji wa Imam Hussein (a.s) na kufungua kesi za kisheria dhidi yao kuwa ni kitendo cha woga, akitaka kusitishwa mara moja kwa kukamatwa kiholela na kuachiliwa kwa wote waliokamatwa.
Serikali ya Punjab imewaita wamiliki wa vibali vya kufanya maombolezo, waandaaji wa vituo vya kutoa huduma za bure (maisha ya Sadaka) na wajumbe wa kamati za ulinzi, na kuwashinikiza watangaze rasmi kujitenga na matembezi ya Arbaeen kuelekea Karbala.