13 Agosti 2025 - 15:49
Kukandamiza waombolezaji wa Imam Hussein (a.s) Punjab ni kitendo cha woga na kinyume na haki za kiraia

Katibu Mkuu wa Baraza la Maimamu wa Kishia nchini Pakistan, Hujjatul-Islam Shabir Hassan Meesami, amelielezea hatua ya Serikali ya Punjab ya kuwashughulikia kwa nguvu waombolezaji wa Imam Hussein (a.s) na kufungua kesi za kisheria dhidi yao kuwa ni kitendo cha woga, akitaka kusitishwa mara moja kwa kukamatwa kiholela na kuachiliwa kwa wote waliokamatwa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Meesami amesema kuwa hatua ya Serikali ya Punjab dhidi ya waombolezaji wa Imam Hussein (a.s) na kufungua kesi dhidi yao ni kinyume na mwelekeo ulioelezwa na Maryam Nawaz.

Ameeleza kuwa, kabla ya maadhimisho ya Arubaini, sera za vitisho, hofu na ukamataji zinaendelea, akibainisha kuwa huko Punjab, hata kwa kuvamia nyumba za watu na kukiuka heshima ya faragha, kunafanyika jitihada za kuzuia uendeshaji wa maombolezo ya Sayyid Shuhadaa (a.s).

Kwa mujibu wa Meesami, hususan katika maeneo ya kusini mwa Punjab, kumefanyika makamatano ya makumi ya watu, jambo ambalo ni kinyume na haki za kiraia pamoja na ahadi za Chama cha Muslim League na Maryam Nawaz, na kunaleta taswira hasi kwa serikali machoni mwa umma.

Katibu Mkuu huyo amesisitiza kuwa katika mwezi wa Muharram, kesi za uongo zimefunguliwa dhidi ya waombolezaji, ilhali kuomboleza kifo cha Sayyid Shuhadaa (a.s) ni haki ya kisheria na ya msingi kwao, na hakuna kizuizi chochote kinachoweza kukubalika katika jambo hilo.

Ameonya kuwa Serikali ya Punjab inapaswa kusitisha mara moja ukamataji wa kiholela na kampeni za vitisho, na kuwaachia huru waombolezaji wote waliokamatwa, ili maadhimisho ya Arubaini ya Imam Hussein (a.s) yafanyike kikamilifu, kwa heshima na kwa amani; la sivyo, wananchi watasimama kulinda haki zao za kiraia na za kidini, na serikali itawajibika kwa madhara yatakayojitokeza.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha