Katibu Mkuu wa Baraza la Maimamu wa Kishia nchini Pakistan, Hujjatul-Islam Shabir Hassan Meesami, amelielezea hatua ya Serikali ya Punjab ya kuwashughulikia kwa nguvu waombolezaji wa Imam Hussein (a.s) na kufungua kesi za kisheria dhidi yao kuwa ni kitendo cha woga, akitaka kusitishwa mara moja kwa kukamatwa kiholela na kuachiliwa kwa wote waliokamatwa.
Baada ya tukio la kusikitisha katika Bandari ya Shahid Rajaei lililosababisha vifo vya makumi ya raia wapenzi wa Iran, Baraza la Mawaziri limetangaza kuwa kesho kutakuwa na maombolezo ya kitaifa kote nchini.