Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la AhlulBayt (a.s) — ABNA — Kufuatia tukio hilo la kusikitisha katika Bandari ya Shahid Rajaei na vifo vya makumi ya raia, Baraza la Mawaziri limetangaza kuwa kesho kutakuwa na maombolezo ya kitaifa kote Iran.
Fatemeh Mohajerani, leo Jumapili tarehe 7 Ordibehesht 1404 (sawa na 27 Aprili 2025), kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wa kijamii X, aliandika: "Baada ya tukio la kusikitisha katika Bandari ya Shahid Rajaei Bandar Abbas, Serikali ya Kumi na Nne imetangaza kuwa kesho (Jumatatu, 8 Ordibehesht) itakuwa siku ya maombolezo ya kitaifa."
Msemaji wa serikali katika ujumbe huo, sambamba na kutoa tena pole kwa familia za waathirika wa tukio hili chungu, alieleza kuwa serikali inafuatilia kwa ukaribu tukio hilo, na pia alitangaza kuhusu safari ya Rais kwenda Bandar Abbas.
Wakati juhudi za mwisho za kudhibiti tukio la Bandari ya Shahid Rajaei zikiendelea, Dk. Masoud Pezeshkian pia aliwasili Bandar Abbas saa chache zilizopita ili kushuhudia kwa karibu hatua zilizochukuliwa na idara husika.
Rais baada ya kuwasili, alitembelea Bandari ya Shahid Rajaei na kushiriki katika kikao maalum cha Kituo cha Usimamizi wa Dharura cha Mkoa kilichofanyika kwa uwepo wa mawaziri na maafisa husika, ili kusikiliza ripoti za moja kwa moja, kutoa maelekezo muhimu ya kuharakisha misaada kwa waathirika, kufidia hasara na kurejesha hali ya kawaida bandarini hapo.
Kwa mujibu wa ripoti na kauli za viongozi husika, wakiwemo Mkuu wa Kituo cha Usimamizi wa Dharura cha Taifa, hadi sasa idadi ya waliopoteza maisha katika tukio hili la kusikitisha imefikia watu 28 na zaidi ya watu 1000 wamejeruhiwa.
Your Comment