Hofu
-
Katika mahojiano na ABNA na mwanafalsafa wa Marekani: Kutoka ‘Medina’ hadi New York; Kushindwa kwa Ukuta wa Hofu Dhidi ya Uislamu Marekani
Profesa Charles Taliaferro, profesa mwandamizi wa falsafa katika Chuo cha Saint Olaf, akitaja wimbi la kampeni za propaganda za kupinga Uislamu nchini Marekani, alisema: “Licha ya kuwepo kwa baadhi ya vipengele vya kupinga Uislamu katika jamii ya Marekani, kuna ishara wazi za heshima, utu, na kukubaliana kati ya Waislamu na watu wengine. Ushindi wa Zahran Mamdani katika uchaguzi wa manispaa ya New York ni tukio muhimu katika kuimarisha harakati za kudhoofisha mazungumzo ya hofu dhidi ya Uislamu.”
-
Hotuba ya 22 ya Nahjul-Balagha: Njia za Kihistoria za Kurejesha Batili!
Katika sehemu hii ya hotuba, Imam Ali (a.s) anasisitiza kwamba vyombo vya habari na mbinu za kisaikolojia ni silaha kuu za Shetani na wafuasi wake katika kujaribu kurejesha dhulma na uongo katika jamii.
-
Usalama wa kisaikolojia katika familia ya Kiislamu؛ mstari wa mbele wa vita vya kifikra
Katika wakati ambapo shambulio za kifikra zinachukua lengo la amani ya nyumbani, familia ya Kiislamu, kwa kuunganishwa kwa imani, upendo na mazungumzo, huunda ngome ya kwanza ya usalama wa kisaikolojia; ni mahali ambapo amani ya kiungu inasimama dhidi ya hofu zinazotokana na vyombo vya habari, na kiroho hubaki kuwa kimbilio la faraja na uhakika wa mioyo.
-
Katibu Mkuu wa Baraza la Maimamu wa Kishia Pakistan:
Kukandamiza waombolezaji wa Imam Hussein (a.s) Punjab ni kitendo cha woga na kinyume na haki za kiraia
Katibu Mkuu wa Baraza la Maimamu wa Kishia nchini Pakistan, Hujjatul-Islam Shabir Hassan Meesami, amelielezea hatua ya Serikali ya Punjab ya kuwashughulikia kwa nguvu waombolezaji wa Imam Hussein (a.s) na kufungua kesi za kisheria dhidi yao kuwa ni kitendo cha woga, akitaka kusitishwa mara moja kwa kukamatwa kiholela na kuachiliwa kwa wote waliokamatwa.
-
Barua ya 18 ya Nahjul Balagha / Onyo kwa Viongozi wote wa Serikali ya Kiislamu
Barua ya kumi na nane (18) ya Nahjul Balagha, ingawa imeandikwa kwa jina la Abdullah bin Abbas, gavana wa Basra wakati huo, lakini inapaswa kuchukuliwa kama onyo kwa viongozi wote wa serikali katika historia yote. Onyo hili linapaswa kuwa mwongozo wa kila mtu anayepewa nafasi au jukumu katika taasisi mbalimbali za mfumo wa Kiislamu.
-
Kukamatwa kwa Mawakala 87 wa Utawala wa Kizayuni katika Mkoa wa Lorestan, Magharibi mwa Iran
Watu hao 87 waliotiwa mbaroni wanatuhumiwa kwa kueneza hofu miongoni mwa raia, kufanya vitendo vya uharibifu, kuwasiliana na mashirika ya kijasusi ya kigeni, na kumiliki vilipuzi.
-
Televisheni yenye kufuata mrengo wa Kizayuni "Iran International" imeanguka, na sasa BBC imechukua nafasi yake
Katika dunia ya sasa, ni vigumu kujua ukweli kamili kwa urahisi, hivyo ni muhimu kuwa na vyombo vya habari vya kuaminika vinavyotumia vyanzo vya haki na kuthibitisha taarifa kabla ya kuzisambaza. Hivyo ndio Vyombo vya kufuatilia na kusikiliza. Na sio kufuata kila chombo cha Habari bila kujua kuwa hiki chombo kinatumiwa na waovu wa uistikbari wa Dunia au la.
-
Je, Mazungumzo Kati ya Mwanamume na Mwanamke Wasiokuwa Mahramu Yamekatazwa kwa namna yoyote ile katika Uislamu?
“Kauli yenye nguvu zaidi ni hii kwamba kusikia (kusikiliza) sauti ya Mwanamke asiyekuwa Mahram, maadamu si kwa ajili ya tamaa, starehe au maslahi, ni jambo linaloruhusiwa (linajuzu). Vivyo hivyo kwa Mwanamke, ikiwa hakuna hofu ya fitina, anaweza kusikika na Wanaume wasio mahram kwake".