Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Katika ufafanuzi wa Hotuba ya 22 ya Nahjul-Balagha, ambayo ni sehemu ya maneno ya Amirul-Mu’minin Imam Ali (a.s) kabla ya vita vya Jamal, Imam (a.s) anaeleza mbinu na malengo ya maadui wa haki, akifichua mikakati ambayo Shetani na wafuasi wake hutumia kuimarisha uovu.
Imam (a.s) anabainisha kuwa Shetani huwafanya wafuasi wake wachochee, wahamashe, watalarishe, na wakusanye jeshi la batili, kwa kutumia njia za kisaikolojia na upotoshaji wa kimtazamo.
Katika sehemu hii ya hotuba, Imam Ali (a.s) anasisitiza kwamba vyombo vya habari na mbinu za kisaikolojia ni silaha kuu za Shetani na wafuasi wake katika kujaribu kurejesha dhulma na uongo katika jamii.
Imam (a.s) anahitimisha hotuba hii kwa kuelekeza njia ya kupambana na harakati hizi za uchochezi na udanganyifu, akisema kuwa suluhisho ni:
- 1_ Kusimama imara bila hofu,
- 2_ Kuwa na yakini thabiti kwa Mwenyezi Mungu,
- 3_ Na kudumu katika imani na msimamo wa kiitikadi.
Mafundisho haya ya Imam Ali (a.s) yametajwa kuwa mwongozo muhimu kwa zama hizi, hususan katika kukabiliana na vita vya kifikra, kisiasa na vya kimitandao (vyombo vya habari) vinavyolenga kueneza uongo na kudhoofisha haki.
Your Comment